Spread the love

 

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amekili kwa kinywa chake kuwa Ligiya msimu huu ni ngumu na hivyo kutoa tahadhari kwa wasimamizi kutoingia kwenye mitego. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Karia ameyasema hayo mkoani Morogoro hii leo tarehe 3, Disemba, 2021 kwenye mkutano wa baraza kuu la Bodi ya Ligi huku kukiwa na ajenda kuu moja ya uchaguzi wa chombo hiko.

Wakati akitoa nasaa ya ufunguzi mkutano huo rais Karia alinena kuwa mara baada ya kuchezwa michezo saba, Ligi tayari imeshaonekana kuwa ngumu hivyo kuitaka bodi ya Ligi kuwa makini katika uwendeshaji wa mashindano hayo na kutoingia kwenye mitego.

“Ligi kama mnavyoona ni ngumu, tucheze kwa uadilifu tusiingie kwenye mitego.” Alisema Karia

Katika michezo saba iliyopigwa mpaka sasa, Yanga imeendelea kusalia kileleni wakiwa na pointi 19, na kwenye nafasi ya pili wakifuatiwa na Simba wakiwa na pointi 17, huku Mtibwa Sugar ikiburuza mkia ikiwa na pointi mbili.

Katika hatua nyingine Karia alisema kuwa kuna haja kwa uongozi wa bodi ya Ligi utakaochaguliwa kuangalia suala la usafiri kwa klabu zinzoshiriki za Ligi Kuu, kupata mabasi yatakayowasaidia kwa safari zao.

“Nitazungumza na uongozi utakaochaguliwa kuhusu usafiri kwa timu za Ligi kuu, kwa kuongea na kampuni za magari ili yaweze kuwapa mabasi timu.” Alisema kiongozi huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *