Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kanisa Katoliki Sri Lanka lasitisha ibada
Kimataifa

Kanisa Katoliki Sri Lanka lasitisha ibada

Spread the love

KANISA Katoliki nchini Sri Lanka limesitisha ibada zake kwa maelezo ya kujihami na shambulio la kigaidi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya nchi hiyo kuonya kwamba, kuna uwezekano wa taifa hilo kukumbukwa tena na shambulio la kigaidi, kama lililotokea siku ya Pasaka tarehe 21 Aprili 2019 katika makanisa matatu na hoteli za kitalii.

Takribani wiki mbili, Kanisa Katoliki limesitisha ibada zake baada ya kutokea kwa tukio hilo lililopoteza maisha ya watu wasio na hatia zaidi ya 250 na kuacha majeruhi kadhaa.

Kanisa hilo limetoa tangazo la kutofanya ibada leo tarehe 2 Mei 2019 kupitia Msemaji wa Mkuu wa Dayosisi ya Kanisa Katoliki mji wa Colombo, Kardinali Malcom Ranjith.

Kardinali Ranjith amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba, wamechukua uamuzi huo baada ya kusikia onyo la serikali.

Kabla ya Kanisa Katoliki kusimamisha ibada zake za Jumapili, lilipanga kufanya ibada Jumapili ya tarehe 5 Mei 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!