Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Mbowe: Msiba wa Dk. Mengi hasara kwa Taifa
Habari MchanganyikoTangulizi

Mbowe: Msiba wa Dk. Mengi hasara kwa Taifa

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Taifa  amesema kuwa, msiba wa Dk. Reginald Abraham Mengi ni msiba kwa taifa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Dk. Mengi ambaye ni mwenyekiti wa kampuni zilizo chini ya IPP Group amefariki usiku wa kuamkia leo tarehe 2 Mei 2019 akiwa Dubai, Falme za Kiarabu.

“Msiba huu ni hasara kwa taifa kutokana na umuhimu wa Dk. Mengi kwa Watanzania. Dk. Mengi ni miongoni mwa watu waliokuwa rafiki kwa vyama vyote vya siasa,” amesema Mbowe.

Kiongozi huyo wa Chadema ametoa kauli hiyo alipokuwa nyumbani kwa marehemu Mzee Mengi, Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa salamu za pole.

Amesema kuwa, Dk. Mengi pamoja na kwamba ni mjomba wake pia rafiki wa vyama vyote vya siasa pia lakini ni rafiki wa masikini, watu wenye ulemavu na kila aina ya makundi ya watu.

Pia wamdishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali waliopo jijini Dodoma kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Dunia, wamesimama kwa dakika moja kutoa ishara ya heshima na kumkumbuka Dk. Mengi.

Nevile Meena, Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri (TEF) akiwa kwenye maadhimisho hayo amesema, kifo cha Dk. Mengi ni pigo kwa tasnia ya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

error: Content is protected !!