December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri ampinga Mbunge CCM

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni

Spread the love

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni amesema, hakuna utaratibu wa askari polisi kutoa fedha zao mfukoni kwa ajili ya chakula cha mahabusu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa leo tarehe 2 Aprili 2019 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Rashid Chuachua (CCM).

Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua, ni lini serikali itarekebisha utaratibu uliopo ambapo askari wanalazimika kutoa pesa zao mfukoni ili kuwapa chakuka mahabusu.

Masauni amesema, utaratibu uliopo ni kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi ina wajaibu wa kuwapatia chakula mahabusu waliopo kororkoroni.

“Ndugu wa mahabusu pia wanaruhusiwa kupeleka chakula kwa mahabusu wao ambao wapo korokoroni,” amesema Masauni.

Naibu Waziri huyo amesema, serikali inatambua uhaba wa vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja uchache wa magari na nyumba za askari.

Amesema, kwa sasa Wilaya ya Masasi ina nyumba za makazi ya askari zipatazo 15 ambazo zinaishi familia 30.

Na kwamba, ni kweli askari wengine 154 bado wanaishi uraiani lakini hata hivyo serikali itaendelea kujenga nyumba za makazi ya askari kwa awamu kwa kadri upatikanaji wa fedha.

error: Content is protected !!