Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya Bunge yashindwa kumhoji Kubenea, alazwa kliniki ya Bunge
Habari za SiasaTangulizi

Kamati ya Bunge yashindwa kumhoji Kubenea, alazwa kliniki ya Bunge

George Mkuchika, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge. Picha ndogo Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

KAMATI ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeshindwa kumhoji mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, baada ya kuona hali yake ya kiafya imezorota, anaandika Dany Tibason.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kampteni George Mkuchika, ameeleza wajumbe kuwa Kamati haiwezi kuendelea na mahojiano na Kubenea kutokana na afya yake kuyokuwa nzuri.

“Kubenea amefika hapa mbele ya Kamati kama ambavyo Spika wa Bunge alivyoagiza kuwa aletwe na polisi. Tumemuona na tumejiridhisha kuwa hatuwezi kuendelea na mahojiano,” ameeleza Mkuchika.

Amesema, “kutokana na hali hiyo, Kamati inaliagiza Bunge kumtibu Kubenea na baada ya hapo, tunaweza kuendelea na mahojiano yetu.”

Kubenea alifika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Maadili leo asubuhi chini ya ulinzi wa polisi.

Alianza kushikiliwa kuanzia jana majira ya saa nne asubuhi baada ya kuripoti kwenye ofisi za Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni.

Kwa sasa, Mhe. Kubenea amelazwa kwenye zahanati ya Bunge mjini Dodoma.

 MwanaHALISI Online itaendelea kukujulisha kila hatua inayoendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!