October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Naibu Waziri atoa neno kuhusu amani nchini

Suleiman Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

NAIBU  Waziri  Nchi,Ofisi ya Rais (TAMISEMI) , Selemani Jaffo amewataka viongozi wa dini kulinda amani ya nchi na kutotumia nafasi zao kutengeneza migogoro ya kisiasa, anaandika Dany Tibason.

Jaffo ametoa  kauli hiyo leo hii wakati akifungua Semina ya Maaskofu na Wachungaji wa Madhehebu mbalimbali katika mkoa wa Dodoma yaliyofanyika mjini hapa.

Amesema kuwa kuna viongozi wa dini ni kiungo muhimu kati ya wananchi na serikali hivyo kazi kubwa waliyonayo ni kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi.

Ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha amani ya nchi pamoja na vinadumishwa  badala ya kuwepo kwa migawanyiko na chokochoko ambazo ambazo zinaweza kulisababishia taifa machafuko.

Akizungumzia kuwepo kwa vikundi mbalimbali vya maombi nchini alisema maombi ni muhimu kwa taifa kwa kuwa yanalenga kuliweka nchi katika utulivu.

Licha ya kusema kuwa maombi ni muhimu zaidi, lakini pia amesema kuwa maombi yafanywe kwa utaratibu ambao utakuwa mzuri usiolenga masuala ya kisiasa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu,  Dk Dismas Mkasa amesema kuwa wameamua kufanya maombi ili kuliombea taifa pamoja na viongozi kwa ujumla.

Akizungumzia matukio mbalimbali ambayo yanajitokeza hapa nchini  kwa lengo la kuwatia wasiwasi wananchi,  Dk.Mkasa amesema kwa sasa ni kipindi cha mpito huku akiwataka wahalifu wote kuachana na tabia hiyo na badala yake wajisalimishe kwa Yesu.

“Tunawataka wahalifu  wote kuhakikisha wanaachana na tabia na vitendo viovu badala yake wajisalimishe kwa Yesu kwani vitendo vinavyotendwa na watu hao siyo vya kiungwana kabisa” amesema Dk.Mkasa.

error: Content is protected !!