Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Jogoo ashtakiwa, kisa kuwika alfajiri
Kimataifa

Jogoo ashtakiwa, kisa kuwika alfajiri

Spread the love

JOGOO mmoja katika kisiwa cha Oléron nchini Ufaransa, jana tarehe 4 Julai 2019 alipandishwa kizimbani akituhumiwa kuwika hivyo kusababisha usumbufu. Vinaripoti vyombo vya kimataifa … (endelea).

Ndege huyo aliyepewa jina la Maurice anayemilikiwa na Corinne Fesseau, ameshtakiwa na majirani walio karibu na nyumba ya mmiliki huyo nchini humo.

Jogoo huyu ambaye mmiliki wake amempatia jina la Maurice, amekuwa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri na malambuno kumhusu sasa yanajadiliwa katika mahakama ya Mji wa Magharibi wa Rochefort, Ufaransa.

Hata hivyo, mmiliki wa jogoo huyo amesema kwamba, jogoo wake anafanya kama ambavyo wanafanya ndege wengine wanavyofanya.

Pamoja na Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux hao kufungua kesi mahakamani, hawakufika ili kusikiliza shauri hilo. Shauri hilo limesababisha jogoo huyo kupata umaarufu zaidi katika kisiwa hicho.

Wafugaji wa kuku kwenye eneo hilo, nao walikwenda mahakamani fuatilia na kusikiliza keshi hiyo.

Lakini jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux walijenga nyumba hiyo miaka 15 kwa lengo la kupumzikia, lakini sasa wamehamia baada ya kustaafu.

Na kwamba, miongoni mwa kuvutiwa na eneo hilo ni utulivu ambao sasa hawaupati baada ya jogoo huyo ‘kusumbua’ kwa kuwika kila ifikapo alfajiri tangu mwaka 2017. Mahakama inatarajia kutoa uamuzi Septemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!