Monday , 29 May 2023
Home Kitengo Michezo Dk. Mwakyembe, wenzake watembelea kituo cha vipaji
Michezo

Dk. Mwakyembe, wenzake watembelea kituo cha vipaji

Spread the love

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameongoza mawaziri wanne, manaibu waziri na wakurugenzi wa idara zinazoshughulikia michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutembelea Shule za Fountain Gate Academy jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ziara hiyo ililenga kuonesha uwekezaji uliofanyika katika kituo cha kuibua, kukuza na kulea watoto na vijana kisoka cha Fountain Gate Academy shuleni hapo.

“Nimewaleta waheshimiwa hawa waone kuwa, kuna taasisi binafsi zimeamua kufanya kile ambacho hakijafanywa mahali popote Tanzania, uwekezaji huu ndio mwarobaini wa soka letu na si kama utaratibu huu wa kubahatisha ushindi” amesema Dk. Mwakyembe na kongeza:

“Nakwenda kufanya mazungumzo na Serengeti Boys waweze kuleta watoto hapa, tunawapoteza wengi kwa kuwaacha bila usimamizi na baadaye wanapotea, hii si sawa hata kidogo.”

Dk. Mwakyembe amesema, ni lazima kuwaandaa vijana ili kucheza timu ya Taifa.

Mahamoud Thabit Kombo, Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale amesema, wamefurahishwa na hatua ya Dk. Mwakyembe kuwapeleka kwenye kituo hicho ili waone uwekezaji wenye lengo la kuinua soka la Tanzania.

“Tumeona jinsi mlivyojipanga kuwezesha soka la vijana wa kiume na wa kike, nitawaalika rasmi kuja Zanzibar ili hii timu ya wasichana ikacheze na timu tutakayoiandaa,” Amesema Waziri Kombo.

Akizungumza kwa niaba ya Fountain Gate Academy, Mkuu wa Shule ya Sekondari shuleni hapo Azimio Dennis Joel amesema, shule hizo zinafanya vizuri kwenye suala la kitaaluma ili iweze kuongoza kimkoa na kitaifa kwa mitihani ya shule za misingi na sekondari.

Mawaziri na manaibu waliotembelea hapo ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Waziri wa Michezo na Utamaduni na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the loveHEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya...

Michezo

Yanga SC. yatwaa ubingwa wa pili mfululizo

Spread the love  KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ya kutwaa ubingwa...

error: Content is protected !!