Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sekta ya Utalii yachangia 17.6% katika pato la Taifa
Habari za Siasa

Sekta ya Utalii yachangia 17.6% katika pato la Taifa

Spread the love

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamisi Kigwangala ameweka wazi kuwa sekta ya utalii ni moja kati ya sekta muhimu nchini katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kutokana na sekta hiyo kuchangia kwa zaidi ya asilimia 17.6. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Amesema sekta ya utalii ni moja ya sekta ambayo inatoa ajira za moja kwa moja laki sita pamoja na zile indirectly zaidi ya milioni mbili nchini ukiacha na kuwa kinara kwa kuchangia kuleta fedha za kigeni kwa asilimia 25.

Kigwangala ametoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano wa Tanapa na wahariri, waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali nchini mkutano uliyohusu kubadilishana mawazo na kuendeleza kukaza utalii na uhifadhi.

Amesema pamoja na kuwa kinara katika kuingiza fedha za kigeni kuliko sekta yoyote ile lakini sekta hiyo ni nyeti katika uchumi wa taifa lakini pia sekta ya uhifadhi kwa ujumla ina faidi pana kwa uhai wa nchi yetu mbali na ufahali wa kuwa nazo sisi kama watanzania.

“Mbali ya kuwa ni Pride (ufahali) wa kuwa na hifadhi zenye hadhi ya kimataifa kama Serengeti na Serui lakini hifadhi hizo ni utajiri mkubwa wa nchi na ukiangalia Tanzania haiwezi kuwa Tanzania bila kuwa na hizi hifadhi ni utambulisho wa Tanzania.

“Sekta hizi mbali na faida hizo nilizozisema za kuleta kipato cha moja kwa moja na kuchangia katika pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 17.6 sekta ya uhifadhi nchini inachangia kwa mfano kwenye kuhakikisha mwanadamu anapata mahitaji yake yote kupitia sekta ya uhifadhi,” amesma Dk. Kigwangala.

Dk. Kigwangala amesema mahitaji hayo ya mwanadamu anayoyapata kupitia sekta ya uhifadhi ni pamoja na kuvuta hewa ya oksijeni inayotokana kwa kiasi kikubwa na jitihada ambazo nchi yetu inazifanya katika sekta hiyo.

Sanjari na hayo amesema usalama wa nchi yetu huko mbeleni tuendako utategemeana na jitihada kubwa zinazoweka kwenye sekta hii, kwani kwa kiwango cha ukuaji wa watu tunaambiwa miaka 12 mbele tutakuwa tumefikia watu milioni 100, sasa ukihesabu miaka 50 mbele tutakuwa tumevuka watu milioni 240.

“Leo tupo watu kati ya milioni 55 au 60 sasa ukiwa unatazama mbali sana na ukiwa sio mbinafsi unaaangalia maisha ya watoto wako na wajukuu zako, utakubaliana na mimi kwamba tutakapofikia idadi ya watu milioni 100, 200 tutakuwa na changamoto kubwa kwenye sekta ya uhifadhi kwa maana pressure itaongezeka na ulinzi utakuwa mkubwa kwenye hifadhi,” amesema Dk. Kigwangala.

 Kutokana na hali hiyo Dk. Kigwangala amesema lazima watu waache kujiangalia wao binafsi kwa kizazi kinachoishi leo hivyo ni kuanza kutambua na kujipa jukumu la kizazi kijacho kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya baadae.

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Allan Kijazi, pamoja na kuishukuru serikali kwa kufungua maeneo mengine ya uhifadhi ili kuyaendeleza, amesema wanachotarajia kutoka kwa wadau hao ni kuweka nguvu za ziada kuyatangaza maeneo haya ndani na nje ya nchi.

Amesema katika kikao hicho watakitumia katika kuwaeleza wahahari pamoja na waandishi kuhusu fursa zilizopo katika vivutio hivyo ili kuhakikisha maeneo hayo yanafahamika na yanakuwa maarufu kwa utalii.

Kijazi amesema miaka 60 iliyopita kumekuwepo na changamoto kubwa kwa upande wa habari lakini kwa sasa imefikia mahala pazuri na kudai kuwa watatumia kikao hicho kuweka mkakati wa pamoja kuona jinsi ambavyo kukuwa kwa sekta ya habari na sekta ya teknolojia ya mawasiliano itakavyoweza kukuza utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!