Jaji mmoja nchini Afrika Kusini amesema, anataka aliyekuwa rais huyo wa Afrika Kusini, kuhukumiwa kifungo gerezani kwa kushindwa kufika mahakamani kujibu madai ya ufisadi.
Zuma alilazimika kujiuzulu kama Rais mwaka 2018. Alidharau ombi la kufika mbele ya tume ya uchunguzi ambayo mwenyekiti wake ni hakimu Ray Zondo.
Jaji amesema, ukaidi wa Zuma kunaweza kusababisha kutotekelezwa kwa sheria na kwamba ataomba mahakama ya juu ya Afrika Kusini, kumhukumu kwa kosa la kuidharau mahakama kwa kitendo chake cha kukaidi wito wa kufika mahakamani.
Zuma amejibu madai hayo na kusema, anaamini kwamba Jaji Zondo alikuwa na upendeleo katika uamuzi alioutoa dhidi yake.
Awali, alikuwa ametaka jaji huyo kujiuzulu kama mwenyekiti wa jopo la uchunguzi wa kesi dhidi yake.
Jaji Zondo alitupilia mbali ombi hilo na kusema anafanya kazi yake bila upendeleo.
Jacob Zuma akabiliwa na mashtaka ya rushwa, na kwamba takribani mashahidi 40 wamemuhusisha aliyekuwa rais na madai ya ufisadi.
Miongoni mwa madai dhidi yake Zuma, ni kwamba wakati akiwa madarakani, aliruhusu familia tajiri ya Gupta kupora mali ya serikali na kushawishi sera na uteuzi wa mawaziri.
Hata hivyo, Zuma na familia ya Gupta wamekanusha madai hayo.
Mahakama ya kikatiba mwezi uliopita, ilitoa uamuzi wake na kusema kuwa Zuma analazimika kufika mbele ya tume hiyo.
Wafuasi wa Zuma wanasema, hawataruhusu afungwe gerezani.
Kufuatia hatua yake ya kutotii agizo la kufika mahakamani Jumatatu, hakimu Zondo amesema, kila mmoja ana haki sawa mbele ya sheria na ikiwa Zuma ataruhusiwa kukiuka agizo la mahakama kutakuwa na athari kidemokrasia.
Zuma hajasema lolote kuhusiana na tukio hilo tangu jaji alipotoa uamuzi huo, lakini awali aliwahi kusema kuwa haogopi kwenda gerezani.
Hata hivyo baadhi ya wanaomuunga mkono waliokuwa wamevaa mavazi ya kijeshi wamekuwa wakiandamana katika eneo la kijijini anakotokea na kuahidi kumlinda.
Zuma alilazimishwa kujiuzulu kama rais mwaka 2018 baada ya kukabiliwa na madai ya ufisadi katika kipindi chote cha miaka 9 alichokuwa madarakani.
Mrithi wake, Cyril Ramaphosa, aliingia madarakani kwa kuahidi kutatua tatizo hilo.
Leave a comment