May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simulizi ya Profesa Jay katika muziki, siasa

Joseph Haule 'Prof. J'

Spread the love

 

UMESAHAU ulipotoka hujui unapokwenda, ukapata kiburi kuona mi nakupenda, nilikuthamini na letu penzi kulienzi na leo siamini kama umenisaliti mpenzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hii ni sehemu ya wimbo wa ‘Nikusaidieje’ ulioimbwa na Profesa Jay akimshirikisha Ferooz. Ni moja ya wimbo ambao Profesa Jay alioutoa mwaka 2005, lakini ukipigwa bado unakonga nyoyo za watu.

Profesa Jay aliyezaliwa tarehe 29 Desemba 1975, amepata fursa ya kuzungumza na MwanaHALISI TV kuhusu safari yake ya maisha, kilichomsukuma kuingia kwenye muziki na baadaye kwenye ulingo wa siasa.

Profesa Jay au jina halisi Joseph Haule, ametoa nasaha kwa wazazi juu ya watoto wao kujihusisha na muziki, jinsi ambavyo wasanii wanaochipukia na walio kwenye ‘game’ wanavyopaswa kuishi ili kudumu kwenye tasnia ya muziki kwa kipindi kirefu.

Unafahamu yeye ni mzaliwa wa Dar es Salaam lakini mwenye asili ya Mikumi mkoani Morogoro na Songea Mkoa wa Ruvuma? Kipi kilimfanya kugombea ubunge Mikumi na si Songea ama Dar es Salaam alikozaliwa? Kwa nini alijiunga na Chadema na si chama kingine?

Hayo na mengine mengi, fuatilia simulizi hii ya Profesa Jay ambaye ni baba wa mtoto mmoja, Lissa (14), aliyebahatika kumpata akiwa na mke wake Grace, aliyefunga naye ndoa mwaka 2017.

error: Content is protected !!