Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Idadi wanaohama kwa hiari Ngorongoro yaongezeka
Habari Mchanganyiko

Idadi wanaohama kwa hiari Ngorongoro yaongezeka

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Christopher Timbuka
Spread the love

 

IDADI ya kaya za wananchi waliokubali kuhama kwa hiari katika Hifadhi ya Ngorongoro, imeongezeka kutoka 296 Juni 2022, hadi kufikia 757 Julai, mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, tarehe 22 Julai 2022, na Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Christopher Timbuka, akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii katika hifadhi hiyo.

Dk. Timbuka, amesema hadi kufikia tarehe 18 Julai, 2022, kaya 757 zenye wakazi 4,344 zimejiandikisha kuhama kwa hiari Ngorongoro, kwenda katika eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili yao, lililopo Msomera mkoani Tanga, huku mifugo iliyoandikishwa ni 8,276.

“Mpaka kufikia juzi kuna kaya 757 zenye jumla ya wakazi 4,344 zimekwisha jiandikisha, katika hizo kaya 495 zimejiandikisha, zimefanyiwa uthamini na kufunguliwa akaunti. Idadi ya mifugo imeandikishwa itaondoka ni 8,276 na katika hizo kaya zilizohama ni 106,” amesema Dk. Timbuka.

Dk. Timbuka amesema, utaratibu wa kuhamisha kaya hizo kwenda Msomera, zinaendelea kufanyika ambapo Serikali inajenga nyumba za makazi yao.

Katika hatua nyingine, Dk. Timbuka amesema, zoezi la kuwahamisha wananchi hao linatarajia kugharimu Sh. 700 bilioni.

“Gharama ya kuhama kwenye hilo eneo (Ngorongoro) ni kubwa, ukichukua idadi ya kaya zilizopo kuna 22,000. Ukipiga hesabu kwa wastani inahitajika Sh. 700 bilioni kuweza kuwahamisha. Lakini wanasema maendeleo ni gharama, hata zikitumika sio tatizo sababu faida itakuwa kubwa,” amesema Dk. Timbuka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!