August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kenyatta: Dunia itatuheshimu EAC tukipata maendeleo kwa umoja wetu

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uhuru Kenyatta amesema wananchi wa Jumuiya hiyo wakiungana na kushirikiana katika maendeleo dunia itawaheshimu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kenyatta amaeyasema hayo leo Ijumaa tarehe 22 Julai, 2022, jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kilomita 14 za barabara ya Arusha-Moshi-Holili na barabara ya mchepuko ya Arusha kilomita 42.4.

Rais huyo ambaye amebakisha siku chache madarakani, amesema endapo nchi hizo zitashairikiana hakuna jambo watakaloshindwa kulifanya na kuwa nchi za mfano Afrika na duniani.

Amesema maendeleo hayo yatakuja endapo wananchi watawaunga mkono viongozi wao akitolea mfano wa namna Watanzania walivyomuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiipokea wadhifa huo wakati wa majonzo na huzuni.

“Mama (Rais Samia) alikuja akashikilia, akawa mjasiri, mchapakazi na kazi mnaiona leo inaendelea na inasonga mbele, kwahivyo ni ishara kuwa tukiwaunga viongozi wetu mkono, tukishikirikiana pamoja kama wananchi wa EAC hakuna jambo linatushinda, tunaweza kubadilisha nchi zetu ziwe nchi viongozi sio tu kwa Afrika bali dunia na tuheshimiwe na dunia kwasababu ya umoja wetu na maendeleo ambayo tunayatekeleza kwasababu ya huo umoja,” amesema Kenyatta.

“Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru dada yetu mama Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu alikuja kuchukua uskani wa nchi ya Tanzania wakati wa majonzi na huzuni…watu walikuwa wanahofu itakuwaje, lakini alituonyesha kwamba msemo wa Kiswahili kweli una maana, Usimwone simba amenyeshewa ifikirie ni paka,” amesema.

Katika hatua nyingine Kenyatta alipongeza jitihada zinazofanywa na nchi hizo kuboresha miundombinu ya usafirishaji inayoziunganisha.

Kenyatta amesema “umuhimu wa miundombinu hauwezi kupuuzwa kwasababu ndiyo msingi wa maendeleo yote, tukiwa kwanza na amani na wananchi wetu wanaishi kwa amani, ya pili ni miradi kama hii kusaidia wananchi kusafiri kupeleka mizigo yao na kujumuika na wenzao wa nchi jirani kwa njia rahisi.

Amesema endapo wananchi wataweza kutembea kutoka Arusha-Holili-Taveta-Voi hadi Mombasa itasaidia wananchi kuwa karibu zaidi na kusaidia biashara ziweze kuimarika, “usafirishaji wa mizigo utakuwa rahisi, nyanya, mboga, mahindi na bidhaa tofauti tofauti zitakuwa zinatembea na kuingia kwenye soko kwetu kule Nairobi kwa njia rahisi,” amesema na kuongeza “na hiyo ni utajiri kwa wakulima Watanzania na wafanyabiashara wa Kenya na njia ya kumaliza umasikini katika nchi zetu.

“Leo ni siku ya furaha tukiungana na viongozi wenzetu wa Afrika Mashariki kuzindua barabara ambayo itakuwa na manufaa kwa mji huu ambao ni moyo wa Afrika mashariki, itapanua miji na kupunguza msongamano na kutuunganisha nchi za Afrika Mashariki,” amesema Kenyatta.

error: Content is protected !!