Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Hospitali Kanda Mtwara yaokoa mamilioni, yajipanga kuhudumia nchi jirani
Afya

Hospitali Kanda Mtwara yaokoa mamilioni, yajipanga kuhudumia nchi jirani

Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mtwara
Spread the love

 

MAMILIONI ya fedha yaliyopaswa kutumika katika kusafirisha wagonjwa kutoka mikoa ya Kusini hadi Dar es Salaam, yameokolewa baada ya Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mtwara, kuanza kutoa huduma za kisasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mtwara, Dk. Hurbert Masigati, baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuzindua hospitali huyo tarehe 15 Septemba 2023.

Amesema hatua ya Serikali ya Rais Samia kupeleka vipimo vya kisasa (CT Scan, MRI), pamoja na wataalamu, imesaidia kuokoa zaidi ya Sh. 200 milioni, baada ya wagonjwa 254 kutibiwa hospitalini hapo badala ya kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Tangu vifaa hivyo vianze kufanya kazi, wagonjwa 102 walihudumiwa na MRI na wale wa CT Scan wako 152 hivyo wagonjwa hao walitakuwa kupewa rufaa kwenda Dar es Salaam na kila mgonjwa ili asafirishwe inagharimu Sh. Milioni moja hivyo zaidi ya Sh. 100 milioni zimeokolewa kwa kuwekwa vifaa hivi pamoja na wataalamu,” amesema Dk. Masigati.

Katika hatua nyingine, Dk. Masigati amesema hospitali hiyo yenye watumishi 224, inajipanga kutekeleza azma ya Rais Samia ya kuimarisha tiba utalii, ikiwemo kwa kuweka vyumba maalum pamoja na mazingira bora ya kuhudumia wananchi na raia wa nchi jirani ikiwemo Msumbiji na Kisiwa cha Morocco.

“Chini ya Serikali ya Rais Samia kupitia Wizara ya Afya, umefanyika uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba vya kisasa ikiwemo vya chumba cha dharura na chumba cha uangalizi maalum (ICU). Kazi yetu ni kutoa huduma kwa ufanisi pamoja na kuimarisha tiba utalii,” amesema Dk. Masigati.

Dk. Masigati ameishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya kwa kuongeza fedha za kununua vifaa tiba na Dawa.

Baadhi ya wananchi walionufaika na hospitali hiyo, wamemshukuru Rais Samia kwa kukamilisha ujenzi wake ulioanzwa na Hayati Dk. John Magufuli, pamoja na kuipa wataalamu na vifaa tiba.

Mwajuma Mohamed amesema “awali tulikuwa tunapata shida kupata huduma, wakati mwingine tulikuwa tunalazimika kutumia fedha nyingi kwenda Dar es Salaam kupata huduma, lakini sasa hivi tunashukuru tunazipata huduma hapa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!