Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hoja sita kutikisa kesi kupinga mkataba wa bandari
Habari za SiasaTangulizi

Hoja sita kutikisa kesi kupinga mkataba wa bandari

Spread the love

HOJA sita zinatarajiwa kutikisa katika usikilizwaji kesi ya kikatiba iliyofunguliwa kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, kwenye uendeshaji bandari nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Hoja hizo zilizowasilishwa jana Jumanne na mawakili wa pande zote mbili, zinatarajiwa kuanza kusikilizwa leo tarehe 26 Julai 2023, katika Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, mbele ya Jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dustan Ndunguru.

Miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kesi hiyo Na. 5/2023, ni iwapo kama kitendo cha kusainiwa na udhinishaji mkataba huo kilikiuka kifungu cha 11(1)(2),  cha Sheria ya Utajiri na Rasilimali Na. 5 ya 2017, ikisomwa pamoja na kifungu cha 5(1), 6 (2)(a),(b), (d) na (i) cha Sheria ya Utajiri wa Asili Na. 6 ya 2017.

Hoja nyingine ni, iwapo kama umma ulijulishwa ipasavyo na kupewa muda wa kutosha kushiriki kutoa maoni yao, kwa mujibu wa sheria wakati wa mchakato wa kuridhia mkataba huo. Nyingine ni iwapo kama vifungu vya mkataba huo vinakinzana na kifungu cha 1, 8, na 28(1) vya katiba ya nchi.

Iwapo kama kifungu cha 2 na 23 cha mkataba huo kinakiuka kifungu cha 25 cha Sheria ya Mkataba ya Tanzania, ni miongoni mwa hoja hizo, huku za mwisho zikiwa ni iwapo pande mbili zilizoingia mkataba zina uwezo kisheria, pamoja na kama mkataba huo ulifuata taratibu za kisheria za Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Tanzania.

Mahakama hiyo mbele ya jopo la majaji hao, wakiwemo Jaji Abdi Kagomba na Ismail Kambona, inatarajia kuanza kusikiliza hoja hizo leo kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Hatua hiyo inajiri baada ya upande wa Serikali, kuondoa mahakamani hapo mapingamizi yake ya awali manne, kupinga usikilizaji wa kesi hiyo, huku sababu ikitajwa ni kuruhusu kesi kusikilizwa haraka kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Mawakili upande wa Serikali, ni pamoja na Wakili Mark Muluambo, Wakili Edson Mwaiyunge na Stanley Kalokola, wakati mawakili wa upande wa walalamikaji wakiwa ni Wakili Mpale Mpoki, Wakili Boniface Mwabukusi na wengine.

Waliofungua kesi hiyo ni mawakili wanne , akiwemo, Alphonce Lusako na Emmanuel Chengula, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Bunge.

Kesi ilifunguliwa muda mfupi baada ya mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Tanzania na Dubai, kuhusu uendeshaji, usimamizi na uendelezaji bandari nchini, kuridhiwa na Bunge.

Waliofungua kesi hiyo wanadai baadhi ya vipengele vya mkataba huo vinakiuka Katiba ya nchi, kupelekwa bungeni kuridhiwa bila kushirikisha umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutoa maoni yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!