Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari Hizi hapa sababu wabunge kuikataa ripoti uchafuzi Mto Mara
Habari

Hizi hapa sababu wabunge kuikataa ripoti uchafuzi Mto Mara

Spread the love

 

BAADHI ya wabunge wameomba uchunguzi huru ufanyike dhidi ya sakata la uchafuzi wa maji ya Mto Mara, baada ya kutoridhishwa na ripoti ya Kamati ya Kuchunguza Uchafuzi wa Mazingira ndani ya mto huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Wabunge hao wametoa ombi hilo jana Jumanne, tarehe 5 Aprili 2022, baada ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Samuel Manyele, kuwasilisha kwa wabunge matokeo ya uchunguzi wake kuhusu suala hilo.

Mbunge Viti Maalumu Mkoani Mara (CCM), Agnes Marwa, ameiomba Serikali iunde tume huru kurudia upya uchunguzi huo, akidai matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo hayaridhishi.

“Niombe Bunge liunde tume huru irudi tena waende wakaangalie tukiwemo sisi wabunge wa eneo husika sababu shida kumuombea kura Rais, wananchi wanaamini Serikali wanataka kuwafanyia vitu ambavyo havieleweki,” amesema Marwa.

Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, ameipinga ripoti hiyo akidai ina mkanganyiko, kutokana na taarifa za matokeo ya uchunguzi huo, kutofautiana na mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo.

“Ukija kwenye conclusion matokeo mnayogundua hayajitoshelezi, nilitaka nipate maelezo kwanza, nini kilitokea. Ukurasa wenu wa 6.3 wa ripoti, Profesa (Prof. Manyele) anafahamu, lazima mapendekezo na conclusion ziwe drawn from observation result, huku kote ukisoma mambo ya ng’ombe hayajitokezi, ghafla yanakuja kujitokeza kwenye mapendekezo,” amedai Prof. Mkumbo.

Prof. Mkumbo amedai “yapo matokeo yenu ya msingi sita katika yale mambo sita yote, ng’ombe hawajitokezi, ila sasa inakuja kujitokeza kwenye conclusion, huwezi kuweka mambo kwenye conclusion ambayo hayajajitokeza kwenye findings, hiyo kwenye utafiti ni contradiction ya kutisha, Prof. anajua.”

Prof. Mkumbo amedai kuwa, uchunguzi uliofanywa katika ubora wa maji ya mto huyo, umebainisha kuwa yana kiwango cha madini ya risasi na zebaki, lakini kamati hiyo haikuzungumzia uwepo wa mchanganyiko wa madini hayo katika hitimisho na mapendekezo yake.

“Ripoti inayofuata inazungumzia water quality (ubora wa maji), inakuja kujitokeza suala la vipimo vya samaki, mmewapima samaki waliokufa wawili tu na mle ndani mkagundua kuna lead content (madini ya risasi) na mercury concentration (mchanganyiko wa zebaki),” amedai Prof. Mkumbo.

Naye Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amehoji kwa nini kamati hiyo haikuwasilisha ripoti zilizofanywa na taasisi nyingine kuhusu uchafuzi huo.

“Tukubaliane kwamba, watu walioko Hospitali ya Ocean Road , zaidi ya asilimia 80 wanatokea Kanda ya Ziwa kwa sababu ya mercury, halafu tumesoma ripoti yenu, tuna ya NEMC, ya Kenya na kuna watu wa Bonde la Ziwa Victoria, ripoti yao imefunikwa haijasomwa hapa. Ni muhimu tupate kamati huru ya uchunguzi,” amesema Waitara.

Amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aingilie kati sakata hilo, akisema wananchi wengi wa Mkoa wa Mara, wanapata maradhi ya saratani kutokana na kutumia maji yenye zebaki.

“Hapa kuna connection ya malalamiko, kulikuwa na shida ya maji ya zebaki kutoka North Mara na huu mto umeanzia kule juu unakuja hapo, hawakwedna kuhoji watu. Kimsingi Bonde la Mto Mara ndiyo kiini cha tatizo. Ikitokea watu wamekufa nani tunampa mzigo?” amedai Waitara.

Waitara amedai kuwa, kamati hiyo imefanya uchunguzi wake pasina kuwashirikisha wabunge wa eneo husika na haikutekeleza majukumu yake ipasavyo katika kubaini kiini cha uchafuzi huo.

“Bahati mbaya hii kamati iliundwa chini ya Makamu wa Rais, tunamheshimu sana, unamuomba Rais aingilie kati,” amesema Waitara.

Akizungumzia maoni hayo, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, amesema Serikali itafanyia kazi mapendekeoz hayo kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kutohatarisha maisha ya wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!