Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesoma barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula, katika Mkutano Mkuu Maalum unaofanyaka leo Ijumaa Aprili Mosi 2022 jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu Dodoma … (endelea).

Katika barua hiyo Mangula ameeleza sababu za umri na utumishi wa muda mrefu ndani ya chama hicho kuwa ndiyo sababu kuu za kuamua kung’atuka.

Mangula emeeleza kuwa sababu hizo zimemfanya ashindwe kutimiza majukumu yake ipasavyo.

“Kufikia tarehe 31 machi 2022 nitatimiza miaka 81 na nimeanza utumishi tangu tarehe moja Januari 1962,” ameeleza Mangula katika barua hiyo kwa Mwenyekiti.

Mangula aliendelea kueleza kuwa alianza kazi ya ualimu katika Chama baada ya kuteuliwa kuwa mwalimu wa siasa 1968 miongoni mwa walimu 75 walioteuliwa na TANU kutoa mafunzo kuhusu siasa ya chama na pia ujenzi wa chama

Mwaka 1969 aliteuliwa na chama kuwa miongoni mwa walimu katika chuo cha TANU Kivukoni na mhariri wa majarida mawili yaliyokuwa yanatolewa na chuo hicho kila baada ya miezi mitatu.

Aliendesha mafunzo ya masafa kupitia redio Tanzania kupitia kipindi cha Fimbo ya Mnyonge na alikuwa mwalimu mshauri katika chuo hicho hadi baadae Kamati kuu ya TANU kumteua kuwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho kwa miaka sita.

Aliteuliwa kuwa katibu wa chama wa wilaya na mkuu wa wilaya na baadae katibu wa chama wa mkoa na mkuu wa mkoa kwa miaka 11 kabla ya kuchaguliw akuwa Katibu Mkuu wa CCM Kkwa miaka 10.

“Nimekuwa makamu Mwenyekiti wa Chama kwa miaka 10 sasa. Huu ni wakati mwafaka wakupanga na kusuka timu ya kuimrasha chama kwajili ya kusimamia utekelezaji wa Ialni ya 2020-2025,” amesema.

Mangula katika barua hiyo na kukishukuru chama kwa ushirikiano waliompa na kuahidi kuendelea kuwa mwanachama mtiifu na raia mwema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *