Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Hizi hapa hoja 10 zinazobeba maridhiano Chadema, CCM
Habari za SiasaTangulizi

Hizi hapa hoja 10 zinazobeba maridhiano Chadema, CCM

Spread the love

 

CHAMA cha Chadema, kimewasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan, mapendekezo 10 yatakayosaidia kutibu madhila yaliyotokea miaka sita iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamelezwa leo Jumatatu, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akielezea ajenda zilizojadiliwa katika kikao cha Chadema na Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika hivi karibuni Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.

“Katika kipindi cha miaka sita iliyopita kupitia ajenda hii tumewasilisha masuala 10 ambayo tunaamini ni vyema yashughulikiwe kama sehemu ya kufungua ukurasa mpya wa haki katika taifa letu. Tunatambua kwamba yako makundi mbalimbali ya wananchi wamepitia madhila na madhara ambayo yanahitaji kushughulikiwa,” amesema Mnyika.

Pendekezo la kwanza lililotajwa na Mnyika, ni uundwaji wa tume ya ukweli na upatanishi, kwa ajili ya kushughulikia mambo ya msingi katika kutatutua madhila ambayo hakuyataja.

Mnyika ametaja pendekezo la pili kuwa ni “kushughulikiwa madhara yaliyotokana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020 na kufungua ukurasa kuhakikisha chaguzi zetu zinakuwa huru na haki kwa mabadiliko ya kitaasisi, kikatiba na kimfumo.”

Katibu Mkuu huyo wa Chadema amesema, pendekezo la tatu ni uhuru wa vyama vya siasa , ikiwemo haki ya kutekeleza shughuli zake ambazo zilizuiliwa katika miaka sita ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Hayati John Magufuli.

“pendekezo lingine ni uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake. Rai yetu imekuwa pamoja na udhaifu wa katiba zetu, sheria zetu, bado kwa miaka 30 iliyopita vyama vimekuwa vikipata haki fulani ambazo utawala wa awamu ya Tano kwa miaka 6 haki hizo zilizuiliwa,” amesema Mnyika.

Mnyika amesema “jambo la nne ni juu ya kufutwa kwa kesi zenye muelekeo wa kisiasa na kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa. Jambo la tano ni kurekebishwa au kufutwa sheria kandamizi katika nchi yetu na jambo la sita ni kushughulikia masuala yanayohusu viongozi wa chama walioshambuliwa, kupotea au kuuawa kwa sababu za kisiasa.”

Mnyika ametaja pendekezo la saba kuwa ni, utafutaji wa namna ya kuziba pengo la kambi rasmi ya upinzani bungeni.

“Jambo la saba, kilichotokea hapo katikati kwenye Bunge ambacho kimesababisha pamoja na mambo mengine kuvurugwa kwa kambi ya upinzani bungeni, kimuundo, kitaasisi na kikanuni. Pamoja na kuwa hatuko kambi rasmi ya upinzani bungeni, lakini tunapotazama mbele kama taifa tunahisi kuna jambo la kurekebishwa,” amesema Mnyika.

Mwanasiasa huyo amesema, pendekezo la nane lililowasilishwa na Chadema kwa Rais Samia, nii hakikisho la usalama wa viongozi na wakimbizi wa kisiasa walioko nje ya nchi kwa sababu za kisiasa.

Miongoni mwa viongozi hao ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu. Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema na mwanahabari Ansbert Ngurumo, walioondoka nchini kwa madai ya kupata vitisho vya maisha.

Mnyika amesema pendekezo la tisa ni kuondolewa bungeni waliokuwa wanachama 19 wa Chadema, akiwemo Halima Mdee, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa, Agnesta Lambart, Esther Matiko, Ester Bulaya na Sophia Mwakagenda.

“Jambo la tisa ni juu ya kuondolewa bungeni waliokuwa wanachama 19 wa Chadema, jambo la kumi ni juu ya kushughulikia madhala mbalimbali kwa ujumla ambayo yamewakumbuka watu na viongozi mbalimbali kwa sababu ya kukandamizwa kwa demokrasia na haki katika taifa letu,” amesema Mnyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!