Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM kuanika mazungumzo Rais Samia, Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

CCM kuanika mazungumzo Rais Samia, Mbowe

Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Watanzania kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kusubiri kuelezwa kile alichozungumza Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa vyama vya kisiasa kwani dhamira zao wote ni njema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Samia kwa nyakati tofauti kukutana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Juma Duni Haji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Mei, 2022 jijini Dodoma kuhusu kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichoketi jana jijini Dodoma, Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kimepokea rasmi na kubariki muendelezo wa mambo hayo ambayo Rais Samia ameanza.

Amesema kikao hicho kilichoketi chini ya Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amesema chama hicho kinatambua mazingira na mahitaji ya hali ya kisiasa na kijamii ndani ya Taifa.

Amesema chama kimeona hiyo ni dhamira ya dhati ya kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kuongeza juhudi za kujenga maridhiano na kuimarisha demokrasia nchini.

Kuhusu jambo lililozungumzwa na Rais Samia na viongozi hao, Shaka amesema lolote jema huwa na chanzo chake.

“Kwenye hili Rais alianza karibu hatua tatu, amekutana na vyama, ameshiriki kuzungumza na viongozi kwenye baraza la vyama vya siasa, ameanza kukutana na viongozi wa kisiasa.

“Tukubaliane muda muafaka utakapofika, Watanzania wataelezwa, kwa sasa wote tusimame kwamba Rais Samia na viongozi wa vyama vya siasa, dhamira zao ni njema na kesho yetu ambayo tunaitafuta ni njema sana kwa Watanzania.

“Walipopafikia na wanapopaendeleza ni pahala pazuri, tuwe na uvumilivu, ustahimilivu, muda utakapofika tutaelezana nini kimezungumzwa… kiko kwenye hatua gani, utekelezaji wake utakwendaje, kwani hata mchicha haukuanza kama mbuyu ulipitia hatua mbalimbali za ukuaji wake kisha kwenda kwa walaji,” Shaka -Dodoma.

Amesema CCM inatambua hatua muhimu na sehemu mojawapo ya kufanikiwa kwenye Taifa letu ni hii ambayo Rais ambayo ameanzisha ya maridhiano na majadiliano.

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Amesema muendelezo wa hilo ni utekelezaji ambao watanzania watanufaika kwa njia moja au nyingine hasa katika misingi ya kuimarisha utawala bora, utoaji wa huduma za kijamii, uchumi na kisiasa.

“Vikao vyote hivyo ni mwanzo mzuri wa kuuendelea maridhiano ya kisiasa lakini majadiliano, mapatano na hatimaye kuwa na Taifa lenye afya bora, umoja, amani na mshikamano pia na kurithi na kuendeleza tunu tulizoachiwa na waasisi wetu.

“CCM tupo tayari kwa mijadala yenye lengo la kuendeleza na kumarisha demokrasia endelevu kwa masilahi mapana ya Taifas letu na wananchi kwa ujumla,” amesema Shaka.

2 Comments

  • Mwanzo ni mzuri!Kusiliza ni atua moja iliyo na maelewano.hongela wote kwa mwanzo huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!