Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto
Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love

 

WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki dunia kwa ajali ya moto iliyotokea usiku wa jana Jumanne, katika ukumbi waliokuwa wanafanya sherehe, ulioko kwenye Wilaya ya al-Hamdaniyah, nchini Iraq. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, takwimu hizo zimetolewa na Naibu Mkuu wa Kurugenzi ya Afya ya Ninawi, Ahmed Dubardani, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo.

Dubardani alisema watu wengine 150 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto, ambapo 50 hali zao kiafya ni tete baada ya kuungua sehemu kubwa ya mwili huku wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Mtandao wa Aljazeera nao umeripoti kuwa, maafa hayo yametokea baada ya jengo kubomoka kufuatia ajali hiyo ya moto.

Hadi sasa mamlaka nchini humo zimetoa wito kwa wananchi kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia majeruhi.

Mazishi ya watu waliofariki katika ajali hiyo yanatarajiwa kufanyika mchana wa leo Jumatano.

Kufuatia tukio hilo, Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani, ametangaza siku tatu za maombelezo.

Hadi sasa mamlaka nchini Iraq hazijaeleza chanzo cha moto huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

Kimataifa

Mateka wa Israel, Gaza kuanza kuachiwa leo

Spread the loveMakubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na vikosi vya...

Kimataifa

Israel, Hamas kusitisha mapigano kwa muda

Spread the loveNCHI ya Israel, pamoja na kikundi cha wanamgambo wa kiislamu,...

error: Content is protected !!