Thursday , 7 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi Desemba mwaka huu, utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini wa awamu ya tatu mzunguko wa pili katika vijiji vyote utakamilika na hivyo kuanza utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme vitongojini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Kapinga amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika Mkoa wa Tabora ambapo katika siku ya pili ya ziara yake amewasha umeme katika kijiji cha Katunda wilayani Uyui mkoani humo.

“Tunatarajia kumaliza kazi ya kusambaza umeme vijijini ifikapo mwezi Desemba mwaka huu, nawahimiza wakandarasi fanyeni kazi yenu kwa uadilifu mkubwa, hatuhitaji kukimbizana juu ya hilo kila mmoja atekeleze jukumu lake kwa maslahi mapana ya taifa letu”, alisema Kapinga.

Kapinga amewaagiza wakandarasi wote nchini kuhakikisha kuwa vifaa vya kufanyia kazi vinakuwepo wakati wote katika maeneo ya miradi ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huo na hivyo kuukamilisha kwa wakati.

Pia, amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukagua vifaa vya wakandarasi ili kujihakikishia kama vipo vyote katika karakana zao ili kazi zifanyike kwa wakati na ziendane na muda wa mkataba uliowekwa.

Vilevile, amewataka REA kuchukua hatua stahiki kwa wakandarasi wote watakaokwenda kinyume na makubaliano ya mikataba ya kupeleka umeme vijijini.

Kapinga amewaagiza REA kuendelea kuwasimamia wakandarasi kwa karibu kwakuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha fedha inazozitoa zinaenda kuwafikishia wananchi umeme kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan.

Naibu Waziri wa Nishati amewasisitiza wananchi kuendelea kusuka nyaya katika nyumba zao ili kujiweka tayari kuunganishiwa umeme pindi utakapowafikia katika maeneo yao na kwamba watu wote watafikiwa na umeme.

Pia alizungunza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tabora na kuwaeleza kuwa watanzania wanataka umeme hivyo wafanye kazi kwa weledi, juhudi na maarifa usiku na mchana kuhakikisha watanzania wote wanapata umeme na kuwatatulia changamoto za umeme zinazowakabili wananchi hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

error: Content is protected !!