Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump
Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love

 

ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia ya ulaghai kwenye shughuli zake za biashara katika muongo mmoja uliopita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mahakama moja mjini New York, imeeleza hapo uamuzi jana Jumanne, kwamba Trump na kampuni yake waliidanganya benki, makampuni ya bima na wengineo kwa kutoa tathimini ya uongo ya mali zake.

Trump alifanya udanganyifu huo, ili kumuwezesha kupata mikataba na mikopo alifanya ulaghai katika shughuli zake za biashara katika muongo mmoja uliopita.

Jaji Arthur Engoron, alitoa uamuzi huo, katika kesi iliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa serikali wa New York, Letitia James.

Aidha, Jaji Engoron ameamuru kufutwa baadhi ya leseni za biashara za Trump kama adhabu na kumuwekea mazingira magumu ya kufanya biashara mjini New York.

Hata hivyo, Christopher Kise, ambaye ni wakili wa Trump amesema, wanaweza kuukatia rufaa uamuzi huo aliouita “upotoshaji wa haki” na usiozingatia ukweli na sheria.

Maamuzi ya kesi hii, yanaweza kuwa na athari kubwa kwa Bw. Trump, anayepambana kutaka kuwania kurejea tena madarakani.

Rais huyo wa zamani wa Marekani, tayari ameshitakiwa kwa kufanya malipo ya kimyakimya kwa nyota wa filamu za ngono kabla ya uchaguzi wa urais wa 2016.

Baraza kuu la mahakama limepiga kura kumfungulia mashtaka baada ya kuchunguza malipo ya dola za Marekani 130,000 kwa Stormy Daniels katika jaribio la kununua kimya chake kuhusu madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Lakini Trump mwenyewe anakanusha kufanya makosa. Yeye ndiye rais wa kwanza au rais wa zamani wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya jinai.

Idara ya Huduma ya siri ya Marekani – ambayo ina jukumu la kuwalinda marais wanaohudumu na marais waliondoka madarakani, itasimamia usalama wa kesi hiyo.

Trump alirekodiwa alama za vidole na kupigwa picha, kama washitakiwa wote katika kesi za uhalifu.

Daniels amesema, alifanya mapenzi na Trump katika hoteli ya Lake Tahoe mwaka 2006, mwaka mmoja baada ya kuoa mke wake wa sasa, Melania.

Katika taarifa yake kwa umma, Trump ameemshutumu mwendesha mashtaka wa wilaya ya Manhattan, kwa kudai kuwa anafanya kazi chafu ya Joe Biden, rais wa sasa wa Marekani.

Trump anakabiliwa na mashitaka mengine ya kuingilia mchakato wa uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza

Spread the loveWaziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu baada ya...

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

error: Content is protected !!