BARAZA la Kukabidhi Mamlaka la Uingereza, limetangaza rasmi mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth II, Charles Philip Arthur George, kuwa mfalme wa taifa hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Charles atakayefahamika kwa jina la Mfalme Charles III, amekabidhiwa mamkala hayo rasmi leo Jumamosi, tarehe 10 Septemba 2022, na Karani wa baraza hilo la siri, Richard Tilbrook, kuwa mfalme wa Uingereza, kiongozi wa Jumuiya ya Madola na mlinzi wa imani.
Baraza hilo la siri limemtangaza ikiwa ni siku moja tangu mama yake, Malkia Elizabeth afariki dunia Alhamisi iliyopita, nchini Scotland alikokuwa anapatiwa matibabu.
Baada ya kutangazwa kushika wadhifa huo, Mfalme Charles ameahidi kuliongoza taifa hilo kwa kufuata nyayo za marehemu mama yake aliyeiongoza Uingereza kwa miaka 70.
Aidha, Mfalme Charles amewashukuru watu ulimwenguni kote waliotuma salamu za rambirambi kwa familia yake kufuatia kifo cha mama yake Malkia Elizabeth.
Hafla hiyo iliyofanyika katika kasri la St. James, jijini London, imehudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo wanafamilia ya kifalme, Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss.
Leave a comment