Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu GEL yataja fursa ziara ya Rais Samia India
Elimu

GEL yataja fursa ziara ya Rais Samia India

Spread the love

WAKALA wa Elimu Nje ya Nchi Global Education Link (GEL) imetaja fursa kem kem ambazo Tanzania itanufaika nazo kupitia  ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan anayotarajia kuifanya nchini India ikiwemo kuimarika kwa utalii tiba nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

GEL imesema India ni nchi inayoongoza duniani kwa utalii tiba hivyo ziara ya Rais Samia itazidi kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali hususan afya.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kwenye ofisi za wakala, jijini Dar es Salaam.

Mollel alisema ziara ya Rais Samia inayotarajiwa kufanyika nchini India kuanzia kesho Jumapili itakuwa na manufaa makubwa kwani Tanzania kwani nchi hiyo inawatalamu bobezi wa kila nyanja na ni nchi inayoongoza duniani kwa utalii tiba.

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akikata keki na mmoja wa wageni waliofika ofisi za GEL kilele cha wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika ofisi za GEL jijini Dar es Salaam

Alisema Tanzania imeshaazimia kuwa kitovu cha utalii tiba kwa nchi  za kusini mwa jangwa la sahara hivyo ziara hiyo itaendelea kuimarisha uhusiano ambao utasaidia nchi kupata watalii wengi wa tiba.

“Kwenye upande wa elimu tutafunguliwa fursa nyingi sana za kwenda kusoma nje India, ufadhili wa wanafunzi utaongezeka, madaktari bingwa na bobezi ambao wanahitaji kubadilishana uzoefu na wenzao wa India fursa zitaongezeka,” alisema Mollel

“Pia tutafanya kitu kinaitwa reverse medical tourism kwa maana kwamba unaweza kuwa na miundombinu ya kutosha lakini ukakosa mabingwa sasa kupitia ushirikiano wa India na Tanzania mabingwa kutoka nchini humo watakuja kuungana na wa kwetu hapa na watatibu maradhi ambayo walikuwa wakienda kutibiwa nje ya nchi,” alisema Mollel

Aidha, alisema kwa uwekezaji ambao umefanywa kwenye sekta ya afya na serikali ya awamu ya sita na uhusiano mzuri wa Tanzania na India, nchi za Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika zitaitegemea Tanzania kwa tiba za kibingwa.

Mollel alisema ziara hiyo pia itafungua milango kwa wanafunzi wa Tanzania waliosoma Shahada ya kwanza ambao wanataka kwenda India kusomea ubobezi kwenye fani ya afya na fani zingine.

Mmoja wa wageni waliofika kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja ya Global Education Link (GEL) akipata zawadi kabla ya kuondoka kwenye hafla hiyo

“India inafahamika dunia nzima kwa ubobezi kwenye sekta ya afya kwa hiyo uwepo wa Rais wetu nchini India utasaidia kuimarisha ushirikiano wa vyuo vikuu vya nchi hiyo na vya hapa nchini ambavyo tumekuwa tukifanya navyo kazi kwa muda mrefu,” alisema

Alisema vyuo vingi vya India vina program za wanafunzi kusomea nchini humo na kumalizia kwenye vyuo vya mataifa mengine hivyo alisema hiyo ni fursa kwa vyuo vya hapa nchini kubadilishana wanafunzi na vyuo vya India.

Wakati huo huo, Molle alisema (GEL),  imefungua dirisha kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchi muda wowote kwa muda wa mwaka mzima kuanzia sasa.

“Kwa wanafunzi waliokosa masomo  vyuo vya ndani na nje ya nchi kuanzia sasa tumefungua dirisha la masomo na watakwenda muda wowote hatutafunga kwa yeyote anayetaka kwenda nje ya nchi aje tutamfanyia mchakato atakwenda ndani ya muda mfupi,” alisema Mollel

Alisema mwanafunzi yeyote ambaye amekosa udahili kwenye vyuo vya ndani asifikiri kwamba amechelewa kwani vyuo vya nje vitaendelea kupokea wanafunzi muda wowote watakaohitaji kwenda nje ya nchi.

Mmoja wa wageni waliofika kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja ya Global Education Link (GEL) akipata zawadi kabla ya kuondoka kwenye hafla hiyo

Kadhalika, Mollel alisema GEL imejipanga kuongeza fursa za masomo kwa watanzania wanaotaka kwenda nje ya nchi kusomea ubobezi kwenye Shahada za Uzamivu (PhD) na Shahada za Uzamili.

Alisema kwa sasa asilimia 90 ya wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi kusoma kupitia GEL ni wa Shahada ya Awali na ngazi za vyeti na Astashahada hivyo kuanzia sasa GEL itajitahidi kuongeza fursa za wanaotaka kusomea ngazi za juu za elimu.

Mbali na hivyo, alisema kutokana na mazingira mazuri ya elimu yaliyowekwa nchini, Tanzania itaanza kupata wimbi kubwa la wanafunzi kutoka nje ya nchi wanaokuja kusoma vyuo vya hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

error: Content is protected !!