Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Faili la mzabuni aliyelizwa latua kwa Waziri Mkuu
Habari za SiasaTangulizi

Faili la mzabuni aliyelizwa latua kwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

SAKATA la mzabuni, Maarifa Nampela ‘aliyelizwa’ Sh milioni 25 na Halmashauri ya wilaya ya Liwale, mkoani Lindi, limetua mikononi mwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbali ya sakata hilo la muda mrefu kutua kwa Waziri Mkuu Majaliwa, ripoti ya mkaguzi wa ndani kuhusu sakata hilo, imeanika undani wa kashfa hiyo na kutoa mapendekezo ya mzabuni huyo alipwe fedha zake.

Katika ripoti yake, mkaguzi wa ndani anakiri kuwepo deni hilo la sh milioni 47.7 na kati ya  hizo, Sh milioni 22.14 zimeshalipwa kwa mzabuni na kiasi kilichosalia ni Sh milioni 22.6 ambazo ndizo zinazoleta mzozo.

Goodluck Mlinga

Mfanyabiashara huyo aliingia makubaliano na halmashauri hiyo kutoa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya wilaya ya Liwale.

Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Majaliwa, zinaeleza kuwa ripoti kuhusu mfanyabiashara huyo na wengine wenye malalamiko kama hayo wilayani Liwale, zimo mezani kwake.

Taarifa za sakata hilo kutua mikononi mwa Waziri Mkuu, Majaliwa zimekuja wakati ambapo Mkuu wa wilaya hiyo, Goodluck Mlinga akimtaka mzabuni huyo aende mahakamani kudai haki yake kwani yeye ameshindwa kumsaidia.

MwanaHALISI Online lilimtafuta Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Zuena Omary kujua msimamo wake kuhusu madai ya mfanyabiashara huyo kama ameshaiona ripoti ya mkaguzi wa ndani, kwanza alisema halijui suala hilo kwa vile ni mgeni na hajawahi kuiona ripoti hiyo ya mkaguzi.

Aliahidi kufuatilia kwa undani sakata hilo na kutoa taarifa, lakini alisema kama mzabuni huyo ana vielelezo na ana mkataba wa kazi hiyo, ana haki ya kulipwa fedha zake.

Hata hivyo alitoa angalizo kuwa kama mfanyabiashara huyo hana mkataba na halmashauri ni ngumu kulipwa, lakini kama kuna watumishi walikiri kuhusika na walikubali kumlipa kasha wakaacha, lazima wamlipe na sheria ichukue mkondo wake.

Watumishi walikiri kuhusika na sakata hili ni Dk. Evaristo Kassanga ambaye alikuwa msimamizi wa mradi.

Wengine waliosimamia mradi huo ulioanza mwaka 2017 na kukubali kulipa fedha hizo ni Halima Kimbwandi ambaye jukumu lake kubwa lilikuwa kupokea vifaa hivyo vya ujenzi, akisaidiana na Paul Mkeyembe  na Anna Mnambale ambaye alikuwa Mahasibu.

Akizungumzia sakata hilo kabla ya kuhamishwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Liwale, Kristina Sekambo alikiri kupata malalamiko ya mzabuni huyo, lakini ofisi yake haina nyaraka zozote kuthibitisha madai yake.

Aliendelea kueleza kuwa ofisi yake imebaini kuwa mzabuni huyo aliingia mkataba na watu binafsi wa kutoa  vifaa hivyo kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hiyo bila mkataba halali na Serikali.

Alisema tayari wahusika ambao ni watumishi wa umma, wamekubali deni hilo na wawili wameshaanza kulipa kupitia akaunti ya mzabuni.

Aliwataja wadaiwa hao kuwa ni Halima Kimbwanda, Anna Mnambale, Paul Mkeyemba na Dk. Erasto Kissanga ambaye wakati huo alikuwa mganga mkuu (DMO) wa hospitali hiyo kabla ya kuhamishiwa Mtama.

Alisema wahusika wawili, Halima na Anna ndio waliokwishatekeleza makubaliano hayo, lakini Dk. Kassanga na Mkeyemba, hawajatekeleza hivyo ofisi yangu inashauri wafanye kama walivyokubaliana.

Alipoulizwa kwanini ofisi yake isitumie nguvu wadaiwa hao ambao ni watumishi wa umma wamlipe mzabuni huyo, alisema ofisi yake itafanya hivyo kama Maarifa atakuja na maombi hayo.

Mfanyabiashara huyo amekuwa akidai kiasi hicho cha fedha kilichosalia kwa takribani miaka sita sasa, bila mafanikio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!