Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Esther Matiko ambana Nape bungeni taarifa za wanasiasa kuvuja
Habari za Siasa

Esther Matiko ambana Nape bungeni taarifa za wanasiasa kuvuja

Esther Matiko
Spread the love

MBUNGE Viti Maalum, Esther Matiko, ameihoji Serikali imejipangaje kutatua changamoto za faragha za watu kuingiliwa mitandaoni kutokana na ukuaji wa matumizi ya akili bandia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Ijumaa, Matiko amesema pamoja na ukuaji Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kuwa na faida, lakini una thari zake kijamii, kiuchumi na kisiasa, hivyo Serikali ina mpango gani kuwajengea uwezo wataalamu wa idara zake nyeti kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hizo.

“Pamoja na kwamba matumizi ya akili bandia yana faida na hasara kiuchumi, kijamii na kisiasa  nitaenda kuzungumzia zaidi mfano wa madhara katika kuingilia faragha za watu. Nataka kujua Serikali imejipangaje kimkakati kupeleka watalaamu mbalimbali mathalani wa mahakama, polisi na idara nyingine nyeti kuweza kuja kukabiliana na madhara hasi ya akili bandia?” amesema Matiko.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema Serikali inaendelea kulinda faragha za watu ambapo hivi karibuni ilitunga sheria ya ulinzi wa taarifa za watu ambapo tume ya ulinzi wa taarifa binafsi imeundwa na imeanza kazi.

Kuhusu wataalamu wa serikali kujengewa uwezo, Nape amesema wizara yake imeandaa bajeti ya fedha kwa ajili ya kuwapa mafunzo watu 500 ndani na nje ya nchi. Pia, amesema Serikali inakusudia kujenga chuo cha masuala ya TEHAMA jijini Dodoma, pamoja na kuanzisha vitu nane nchi nzima ili kutoa mafunzo ya kukabiliana na akili bandia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!