SERIKALI imetakiwa kuhakikisha maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye mitaala mipya ya elimu ili kupata wahitimu watakaoweza kushindana katika soko la ajira la kimataifa hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo ulitolewa jana tarehe 8 Februari 2024 na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, bungeni jijini Dodoma.
Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema ajira zenye uhitaji wa watu ulimwenguni ni zile zinazohusiana na masuala ya sayansi na teknolojia, ikiwemo za ukuzaji program (Software development), uchambuzi wa habari za kisayansi za data (Data scientific information analyst), uchambuzi na usimamizi wa akili bandia (Management analysis artificial intelgence) na uuguzi.
Amesema ili Serikali iandae watanzania watakaofanikiwa kuzipata kazi hizo ni lazima ibadilishe muundo wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), ili iwe taasisi badala ya tume.
“Nikiangalia ajira ambazo zinapatikana na kazi namba dunia inayotafuta watu ni software development na manesi unajua COVID-19 walikufa wengi sana hivyo dunia wanatafuta manesi wenye uwezo, hizi ndizo kazi duniani ili tuzipate lazima na taasisi ya sayansi la sivyo hatutavuka,”amesema Prof. Muhongo.
Leave a comment