Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Biashara Bodi CRB, ERB zamshukia mkandarasi Kagera
Biashara

Bodi CRB, ERB zamshukia mkandarasi Kagera

Spread the love

Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), zimetoa onyo kali kwa Mkandarasi ECIA Company Ltd, anayejenga barabara ya Kanyinabushwa-Mbale “A” Wilayani Misenyi mkoani Kagera kutokana na kutozingatia kanuni, sheria na miongozo ya shughuli za majenzi nchini.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na vyombo vya Habari Jijini Dodoma, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Mhandisi Rhoben Nkori amesema timu ya pamoja ya CRB na ERB baada ya kuchunguza ujenzi wa kalvati lililobomoka kabla ya ujenzi wake kukamilika imebaini kuwa uharibifu huo ulisababishwa na matumizi ya malighafi hafifu kinyume cha matakwa ya mkataba na kuruhusu kupita kwa vyombo vya moto katika barabara hiyo kabla ya Kalvati lililojengwa kukamilika.

“Kwa mujibu wa sharia ya usajili wa mkandarasi sura ya 35 ya mwaka 2002 tumempa onyo kali Mkandarasi ECIA Company Limited na endapo akirudia tena kosa la aina hiyo atachukuliwa hatua kali zaidi”, alisema.

Naye Msajili wa Bodi ya Wahandisi Mhandisi Benard Kavishe amesema ERB inawataka wakandarasi wote wahakikishe wanaajiri wahandisi wenye sifa ili kusimamia miradi kikamilifu na hivyo kuleta usalama kwa watumiaji.

Amesema kwa mujibu ya sharia ya Usajli wa wahandisi Sura ya 63 ya mwaka 2012 ni kosa kwa mtu asiyekua na taaluma ya uhandisi na asiyesajiliwa na bodi ya usajili ya wahandisi kutojihusisha na shughuli za kihandisi.

“Tunatoa wito kwa wananchi na wakandarasi wote nchini, kuhakikisha kuwa shughuli zote za ujenzi zinasimamiwa na wataalamu wenye weledi na waliosajiliwa ili kuleta tija na ufanisi, na wote watakaobainika kukiuka sheria hizo Bodi haitosita kuwachukulia hatua za kisheria”, alisema.

Uchunguzi huo unafuatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wa tarehe 17 Januari mwaka huu kufuatia kadhia ya kubomoka kwa kalvati katika barabara ya Kanyinabushwa-Mbale “A” Wilayani Misenyi Mkoani Kagera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

Biashara

Vuna mapene hadi Mil 400 ukicheza Expanse Tournament 

Spread the love  Promosheni ya kuvuna mahela ya Meridianbet bado inaendelea kusaka...

error: Content is protected !!