Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Eric Omondi mbaroni kwa kuongoza maandamano Kenya
Kimataifa

Eric Omondi mbaroni kwa kuongoza maandamano Kenya

Spread the love

 

MCHEKASHAJI maarufu kutoka nchini Kenya Eric Omondi ametiwa mbaroni na jeshi la polisi nchini humo, kwa tuhuma za kuongoza kundi la vijana katika maandamano nje ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Omondi ameongoza maandamano ya kundi la vijana kwa lengo la kupaza sauti wakiitaka serikali kuhakikisha inashusha gharama za maisha nchini humo.

Vijana hao walikuwa vifua wazi huku wakiwa wamevalia minyororo shingoni na kushikilia mabango yenye jumbe mbalimbali za kuonesha kutoris=dhishwa na ugumu wa maisha.

Kutokana na maandamano hayo, inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya biashara katika eneo linalozunguka Bunge, zililazika kusitishwa kwa muda kutokana na hofu ya usalama.

Inadaiwa kuwa polisi wamelazimika kuingilia kati maandamano hayo na kuwaamuru waandamanaji hao kutawanyika, bila mafanikio, jambo lililowalazimu kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na kumkamata kiongozi wa maandamano hayo mchekeshaji Omondi na baadhi ya waandamanaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!