Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaondoa ukomo uhai wa vitambulisho vya Taifa
Habari Mchanganyiko

Serikali yaondoa ukomo uhai wa vitambulisho vya Taifa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imetangaza kuondoa ukomo wa uhai wa vitambulisho vya taifa vilivyo na tarehe ya kuisha muda wake wa matumizi ili kuondoa usumbufu kwa wananchi kuhuisha vitambulisho hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaan … (endelea). 

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mapitio ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu za mwaka 2014.

Awali vitambulisho vya Taifa vilikuwa na ukomo wa miaka 10 na baada ya hapo mwananchi angelazimika kwenda kujisajili upya kupata kitambulisho.

Aidha, Waziri Masauni amesema kuwa amefanya marekebisho ya kanuni ya 16 na Jedwali la pili la kanuni hizo ambapo pamoja na mambo mengine itampa uwezo Waziri mwenye dhamana kufanya marekebisho ya ada zilizopo kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha.

Katika hatua nyingine Masauni amesema hadi kufikia Januari mwaka huu 2023, takribani watu milioni 1.6 hawajachukua vitambulisho vyao vya Taifa.

Amesema jumla ya vitambulisho 11, 295,308 vimezalishwa, huku vitambulisho vilivyochukuliwa na wananchi vikiwa ni 9,687,708 tu.

Aidha amesema wananchi 19,926,015 wamepewa namba za Vitambulisho vya NIDA na wote wanastahili kupata huduma katika taasisi zote nchini sawa na watu wenye vitambulisho vya NIDA.

1 Comment

  • KAMA BADO ANAAMINI “UTI WA MGONGO NI KILIMO” BASI “LIKE FATHER, LIKE SON” HASA KWENYE MAISHA YA “KIFO HAKINA HURUMA” / KIFO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!