Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DP World mbioni kuanza kazi Bandari ya Dar es Salaam
Habari za Siasa

DP World mbioni kuanza kazi Bandari ya Dar es Salaam

Spread the love

KAMPUNI ya Dubai Port  World kutoka Imarati ya Dubai, inatarajiwa kuanza uendeshaji wa maeneo waliyokodishwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kwenye robo ya kwanza ya 2024 endapo itakamilisha taratibu za kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 9 Januari 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa, amesema taratibu za kisheria ambazo DP World hajakamilisha ni ukataji leseni ya kuendesha bandari,  pamoja na uundwaji wa kampuni ya pamoja kati yake na Serikali, kama makubaliano yao yanavyoelekeza.

“Kwa hiyo mategemeo yetu ni kwamba tutaanza katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2024. Sisemi mwaka huu wa kifedha, utaanza nusu hii ya pili ya mwaka huu wa kifedha. Lakini kama taratibu hizi zikikamilika mapema ataanza robo ya kwanza ya mwaka huu lakini naahidi kwamba kabla ya kuanza tutatoa taarifa rasmi ya tarehe ambayo ataanza kazi hapa,” amesema Mbossa.

Aidha, Mbossa, amesema mazungumzo kati ya TPA ambayo inaiwakilisha Serikali ya Tanzania na DP World yanaendelea ili kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuanza kuyafanyia kazi kabla ya makabidhiano ya mwishohayajafanyika.

“Lakini niwaambie makabidhiano ni shughuli ambayo inahitaji umakini mkubwa kwa sababu ndio unataka kuwa mwendeshaji kutoka serikalini basi lazima ujali kila kitu kinachotakiwa kwa sababu kama mnavyojua shughuli zetu sio tu tunazifanya kwa mujibu wa sheria lakini pia zinatakiwa zifuate taratibu zote na zikaguliwe baadae, kwa hiyo tusingependa kuingia katika kitu ambacho hatujakifanya vile ambavyo inatakiwa,” amesema Mbossa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

error: Content is protected !!