Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy Semu amechukua fomu kwa ajili ya kugombea uongozi wa chama hicho taifa, baada ya Zitto Kabwe, kutangaza kung’atuka. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 18 Februari 2024, katika makao makuu ya ACT-Wazalendo, jijini Dar es Salaam, Semu aliyesindikizwa na wafuasi wake, amechukua fomu hiyo

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Semu ametaja mambo matatu yaliyomsukuma kutaka kuvaa viatu vya Zitto, endapo wajumbe wa mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo, watamchagua katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Machi mwaka huu.

“Jambo la kwanza naamini katika uongozi wa pamoja, utumishiw wa watu na kuonesha njia ili kutimiza Kwa ukamilify malengo makubwa ya taasisi kuelekea ndoto ya ACT-Wazalendo. Mmenipima kwenye majukumu mbalimbali mlioniamibi kwayo Kwa miaka hii nane,” amesema Semu.

Ametaja kazi alizofanya  katika nyadhifa mbalimbali alizokabidhiwa ndani ya ACT-Wazalendo, ikiwemo kukivusha kwenye mawimbi ya Kidemokrasia, mawimbi ya kufutuwa usajili wa chama.

“Nilipokuwa Katibu Mkuu 2017-2020, nimekivusha chama kwenye mawimbi ukandamizaji wa kidemokrasia, mawimbi ya kufutiwa usajili na hata kwa pamoja kuvunja rekodi za usimamizi wa kifedhana kuwa chama kinachokua kwa kasi kuliko vyote Afrika.

“Nikiwa Makamu Mwenyekiti Bara mwaka 2021 nilipewa jukumu jingine la kukaimu Uenyekiti wa  chama baada ya kutangulia mbele za haki kwa aliyekuwa mwenyekiti wetu mpendwa Maalim Seif Mungu amrehemu na kukakikisha anapatikana Mwenyekiti mwingine kwa mfumo wa kidemokrasia kama matakwa ya katiba yetu ya chama,” amesema Semu.

Kuhusu jambo la pili, Semu amesema ” ninaamini katika wajibu mkubwa wa vyama shindani, uwepo wa chama hiki katika siasa za vyama vingi umeendelea kutoa tafsiri halisi ya nini wajibu wa vyama vya siasa katika siasa za ushindani katika kuleta sera za kimapinduzi za kubadilisha kabisa hali ya umaskini wa watu wetu, sera mbadala zenye tija, kuendeleza siasa za masuala ambazo chama chetu kimejitofautisha nazo na kuendelea kuwa kimbilio na sauti kuu ya kutafuta maisha ya neema kwa kila mtanzania.”

“Ninataka kuongoza ndoto hii ya ACT Wazalendo kufikia mabadiliko chanya, ya kweli, ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Nafasi nilizo watumikia za Katibu wa Sera na Utafiti na sasa Waziri Mkuu Kivuli zimeendelea kunipika na kunipa uzoefu mkubwa ndani na nje ya nchi,” amesema Semu.

Jambo la tatu alilolitaja Semu ambalo atalifanya endapo atachaguliwa ni kuiimarisha ACT-Wazalendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!