Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa ailaumu Serikali kuficha kuugua kwa Hayati Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa ailaumu Serikali kuficha kuugua kwa Hayati Magufuli

Spread the love

 

BALOZI Mstaafu,Dk. Wilbrod Slaa, ameilaumu Serikali kwa kuchelewa kutoa taarifa za kuugua wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, akisema kitendo hicho kiliwanyima Watanzania fursa ya kumuombea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 25 Machi 2022, jijini Mwanza, akihutubia katika kongamano la urithi wa falsafa ya Magufuli, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.

“Tukio hilo(kifo cha Magufuli) pia linikumbushe uchungu mkubwa kidogo nilioupata, labda Serikali kwenye hili mtusikilize. Serikali mmetunyima Watanzania nafasi ya kumuombea baba yetu tunayempenda kwa Mungu katika kipindi kigumu cha maisha yake alipokuwa anaumwa kwa kutuficha taarifa,” amesema Dk. Slaa.

Mwanasiasa huyo nchini Tanzania ambaye kwa sasa hana chama cha siasa, amesema Watanzania walipaswa wajulishwe juu ya suala hilo, ili wamuombee wakati anaumwa, huku akitoa tahadhari kwamba tukio hilo liwe fundisho.

“Mwisho tunakuja kuambiwa amefariki, lakini tunajua alikuwa anaumwa kwa siku kadhaa kabla ya pale. Tulitakiwa tujulishwe kwa nini unawanyima Watanzania hao fursa na nafasi ya kumuombea? Hii iwe fundisho imetokea hatuwezi kurudisha nyuma. Serikali muwe makini hatuwezi kuhodhi imani ya mwanadamu hata kama ni kiongozi,” amesema Dk. Slaa.

Akielezea alivyomjua Magufuli enzi za uhai wake, Dk. Slaa amesema alikuwa kiongozi asiye na woga, aliyefanikiwa kuunganisha wananchi bila kujali yale yaliyokuwa yanawatenganisha.

Dk. Slaa amesema kuwa, muitikio wa mamilioni ya watu kushiriki ibada za kuuaga mwili wa Magufuli, ulifuta dhana iliyojengwa na baadhi ya watu kwamba alikuwa na maadui wengi.

Balozi Dk. Wilbroad Slaa

Aidha, Dk. Slaa amesema Magufuli alikuwa kiongozi asiyependa changamoto, na hilo alilishuhudia pale alimpoteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, 2017 bila ya kupata ridhaa yake.

“Aliniteua akanipigia simu kunieleza kuwa ameniteuwa, lakini kibali changu hana. Hapa unapata picha gani? Hayati Magufuli ni mtu ambaye anataka vitu vyake viwe vya uhakika, si wa kutegemea challenge (changamoto), hataki challenge na ndivyo nilivyojifunza hata baadae,” amesema Dk. Slaa.

Amesema, nchi za Afrika zilimheshimu Magufuli kutokana na uzalendo wake huku akisema alikuwa kiongozi ambaye haogopi kuchukua hatua na mpenda demokrasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!