Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Nchimbi ampigia chapuo Samia kwa vyama vya ukombozi Afrika
Habari za Siasa

Dk. Nchimbi ampigia chapuo Samia kwa vyama vya ukombozi Afrika

Dk. Emmanuel Nchimbi
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel Nchimbi, amesema Rais Samia ana dhamira ya dhati katika kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa Mataifa ya Kusini Kwa Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Balozi Nchimbi aliyasema hayo jana Jumanne, katika Mkutano wa 11 wa makatibu wakuu wa vyama vya rafiki vya ukombozi wa Kusini mwa Afrika, unaoendelea nchini Zimbabwe.

Katika hatua nyingine, Balozi Nchimbi alisema CCM inajivunia juu ya uongozi wa  Rais Samia aliyetimiza miaka mitatu madarakani tarehe 19 Machi mwaka huu, kufuatia kifo cha mtangulizi wake Hayati John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021.

“Kwa kweli ninajivunia sana Rais Samia si Kwa sababu tu Mimi ni mpigania haki za Wanawake, bali kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa uongozi mzuri anavyoendelea kuingiza nchi yetu. Kutokana na hilo CCM inajivunia uongozi wake na wananchi wote kwa ujumla tunajivunia kuongozwa na Rais Samia Kwa uwezo wake aliouonesha Kwa miaka mitatu hii,” alisema Balozi Nchimbi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!