Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Nchimbi aanza na wapinzani
Habari za Siasa

Dk. Nchimbi aanza na wapinzani

Dk. Emmanuel Nchimbi
Spread the love

KATIBU Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi, ameanza kazi kwa kutuma salamu kwa vyama vya siasa vya upinzani, akiwataka waache tabia ya kususa katika mazungumzo ya kutafuta maridhiano juu ya masuala mbalimbali yanayohusu nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Nchimbi ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Januari 2024, akizungumza katika mkutano jijini Dodoma.

“Tunajua kwamba tunao wajibu na utashi wa kisiasa wa kutumikia nchi, tunajua wapinzani hao wanayo nafasi ya kikatiba ya kushiriki kujenga nchi ndiyo maana tunawabembeleza jamani tukae tuzungumze na sisi hatutasusa kuzungumza kila tutakapokuwa na kitu kimekwama tutataka tuzungumze,” amesema Dk. Nchimbi.

Mtendaji huyo wa CCM amesema uamuzi wa chama chake kuketi mezani na wapinzani haimaanishi kama ni dhaifu, bali wameamua kuwa waungwna.

“CCM mafanikio yote tuliyonayo pamoja na ukweli kwamba tutashinda kwa kishindo lakini hatukubali kuwa na kiburi. Hatukubali kuwa na kiburi bado tutaendelea kuwa wanyenyekevu, tunapowaambia wapinzani tunawaomba jamani tukae tuzungumze sio maana yake kwamba wana nafasi ya kushinda hawna ni uungwana wetu kwa sababu tunajua wajibu wetu kutumikia nchi yetu,” amesema Dk. Nchimbi.

1 Comment

  • Nchi zilizoendelea wanapokezana ndiyo maana wanaendelea. Mexico walikwama kwenye miaka 71 ya PRI. Wapinzani walipoingia walikaa miaka 15 tu lakini nchi iliendelea sana kwa muda huo mfupi. PRI waliposhinda waliwajibika.
    Wakati umefika wa kuwaondoa wababaishaji…wawe upinzani au CCM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!