MMOJA wa wakulima katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Machite Mgulambwa ameiomba serikali kupunguza masharti ya upatikanaji wa vibali vya kuuza mazao nje ili wakulima wadogo nao wapate fursa kuuza mazao yao nje bila vikwazo. Anaripoti Danson Kaijage, Kongwa (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Online amesema pamoja na juhudi za serikali kubana mianya holela ya upelekaji wa mazao ya chakula nje ya nchi, bado wakulima wadogo wapo katika wakati mgumu kwa kushindwa kupata vibali hivyo kutokana na masharti magumu.
Mkulima huyo ameeleza kuwa ili mkulima ni kuuza aweze kujikwamua kimaisha lazima auze mazao hasa ikizingatiwa anatumia rasilimali fadha nyingi, muda na nguvu katika kulima.
“Sisi wakulima tunaishauri Serikali kuona namna ya kulegeza masharti ya kupata vibali, si kwamba vibali havipatikani lakini mlolongo wake ni mrefu mno.
“Tunalima ili tuuze na tujikwamue kumbuka mkulima anatumia gharama kubwa wakati wa kilimo kuanzia kukodisha shamba, kukodisha trekta, pembejeo pamoja na vibarua.
“Sasa tunapojikuta tunashindwa kuuza mazao yetu nje kwa kushindwa kupata wepesi wa kupata vibali, ni wazi kuwa mkulima hawezi kufurahia kilimo na matokeo yake anajikuta katika madeni” amesema Machite.
Leave a comment