Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango kumwakilisha Samia katika mkutano wa dharura wa SADC, Zambia
Habari za Siasa

Dk. Mpango kumwakilisha Samia katika mkutano wa dharura wa SADC, Zambia

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango
Spread the love

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango anatarajiwa kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Lusaka, Zambia tarehe 23 Machi 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Makamu wa Rais ataondoka nchini tarehe 22 Machi 2024 kushiriki Mkutano huo ambao agenda kubwa ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi za SADC, hususan katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo utatanguliwa na Mikutano ya maandalizi ya ngazi za Wataalam ambayo ilianza tarehe 17 Machi 2024 na itakamilishwa na Mikutano ya Makatibu Wakuu na Mawaziri itakayofanyika tarehe 22 Machi 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ataungana na Mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama katika Mkutano huo muhimu.

Tanzania kama mwanachama wa SADC na ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani katika nchi za Msumbiji na DRC inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za Mkutano huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!