Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango ataka ubunifu kusaka suluhu changamoto za kifedha
Habari za Siasa

Dk. Mpango ataka ubunifu kusaka suluhu changamoto za kifedha

Spread the love

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amesema taasisi za kifedha za kikanda na kimataifa zinapaswa kujishughulisha zaidi katika kubuni na kutoa masuluhisho ya kifedha ili kuunga mkono azma ya nchi za Afrika  ya kuharakisha maendeleo ya rasilimali watu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Makamu wa Rais amesema hay oleo tarehe 25 Julai 2023 wakati akihutubia viongozi mbalimbali wa Afrika akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.

Makamu Rais Dk. Philip Mpango akisalimiana na Mke wa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela mama Graca Machel wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu leo trehe 25 Julai 2023.

Amesema uwekezaji katika Rasilimali watu ni wa muda mrefu hivyo unahitaji ufadhili wa gharama nafuu kutoka taasisi hizo za fedha za kimataifa.

Aidha, Makamu wa Rais ametoa wito kwa taasisi za mafunzo na elimu kuhakikisha zinasaidia bara la Afrika kuimarisha uwezo wa wazawa katika kusimamia na kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo.

Amesema Bara la Afrika linatumia rasilimali nyingi za kifedha katika kutafuta maarifa na rasilimali watu kutoka nje ya bara hilo kwa ajili ya kutumia maliasili zilizopo. Ameongeza kwamba kutokana na umuhimu wake taasisi za mafunzo barani Afrika zinapaswa kushirikiana na kutafuta suluhisho ya changamoto zinazolikabili bara hili.

Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa mkutano huo kutafuta njia bora zaidi ya kuihamasisha sekta binafsi kushirikiana na serikali katika kuzalisha rasilimali watu iliyo bora kwa kuwa sekta binafsi ni wanufaika wakubwa wa maendeleo ya rasilimali watu.

Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa Bara la Afrika na wadau wa maendeleo kuwekeza zaidi katika elimu, afya, lishe, maendeleo jumuishi pamoja na ulinzi wa jamii.

Ametoa wito kwa wahudhuriaji wa mkutano huo kujadili na kupata sera za kibunifu zitakazosaidia katika kuboresha maendeleo ya rasilimali watu na kuwapa uwezo idadi kubwa ya vijana inayoongezeka barani Afrika.

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaboresha rasilimali watu kwa kuwekeza katika sekta za elimu, afya na kilimo ikiwemo kuongeza bajeti na kuhakikisha miundombinu rafiki katika sekta hizo.

Amesema hatua zilizochukuliwa zimesaidia katika kupata matokeo chanya ikiwemo ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule kutoka asilimia 85 mwaka 2015 hadi 97 mwaka 2021 huku kiwango cha wanaohitimu elimu ya msingi kufikia asilimia 100 mwaka 2022 kutoka asilimia 80 mwaka 2015.

Ameongeza kwamba vyuo vya ufundi nchini Tanzania vimejengwa katika mikoa 30 kati ya 31 pamoja na kuongezeka kwa uwiano wa kijinsia wa 1:1 katika kupata elimu.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amesema Tanzania inapitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Sheria ya Elimu na Mitaala mapitio yanayolenga kuboresha mfumo wa elimu ili kukidhi ukuzaji wa vipaji, ujuzi wa vitendo, umahiri wa kujenga, fikra chanya na kuwafanya wahitimu kutambua teknolojia ya hali ya juu.

Amesema jambo hilo linatarajiwa kuongeza tija kwa vijana, ushindani katika soko la ajira pamoja na kuwaandaa wahitimu kuwa wabunifu wa kazi kwa kujiajiri zaidi kuliko kuajiriwa.

Pia amesema katika jitihada za kuimarisha rasilimali watu juhudi zinaelekezwa katika utoaji wa mafunzo, mapinduzi ya kidijitali, kuongeza utoaji wa huduma za jamii pamoja na usambazaji wa nishati ya umeme ili kufikia vijiji vyote.

Vilevile, kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kwa kutambua ongezeko la wanaotumia intaneti kutoka asilimia 36.5 mwaka 2015 hadi asilimia 49 mwaka 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!