Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TCRA yazuia vifaa 108,395
Habari Mchanganyiko

TCRA yazuia vifaa 108,395

Spread the love

JUMLA ya simu 108,395 na vifaa vingine vya mawasiliano vimezuiliwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kuhusishwa na vitendo vingi vya jinai, ikiwa ni pamoja na ulaghai, vitendo vya udanganyifu, kuibiwa, na kuripotiwa kwa wizi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabiri Bakari, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma hivi karibuni, kwamba mamlaka imekuwa macho katika kutambua vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa katika vitendo vya udanganyifu na kuzizuia Namba za Kitambulisho cha Kimataifa cha Vifaa vya Mkononi (IMEI) za vifaa hivyo.

Dk Bakari alisema wamefanikio ya kuzuia matumizi ya simu feki, zinazofanana, zilizoripotiwa kuibiwa, kupotea, au kuharibika, pamoja na vifaa vya mkononi visivyoruhusiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

“Kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023, jumla ya IMEIs 108,395 zilizuiwa na mifumo yetu, ambazo zilikuwa zimehusishwa na visa vya wizi au kushiriki katika shughuli za jinai.

Hii sio tu imechangia kupunguza matukio ya wizi lakini pia kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora vya mawasiliano sokoni,” alisema.

Bakari alisema mwezi Novemba mwaka jana, TCRA ilatangaza kuzuiwa kwa namba 52,000 za simu, ikiwa ni pamoja na namba za wadanganyifu na kuanzia Julai 2021 hadi Septemba 2022, jumla ya IMEIs 52,087 zilizuiwa kutokana na kuripotiwa kuibiwa, kupotea, au kuhusika katika shughuli za jinai.

“Moja ya nyenzo ambayo TCRA hutumia katika mchakato huu ni Rejista Kuu ya Usajili wa Vifaa ambayo inawezesha ukaguzi wa vifaa vyote vinavyounganishwa na watoa huduma, kuhakikisha kufuata viwango vya kimataifa na usalama kwa watumiaji.

Alisema TCRA imekuwa macho katika kutambua simu za udanganyifu zinazoingia nchini, ambapo kumekuwa na kupungua kwa visa vya simu za udanganyifu kutoka mwaka 2020 hadi Juni 2023 na Septemba 2022 kulikuwa na visa vichache.

“Tuna mfumo wa kusimamia na kudhibiti mawasiliano yote na kuchambua data mbalimbali zinazopita kupitia mitandao ya mawasiliano,”alisema.

Alisema mfumo huu hupokea taarifa kutoka kwa watoa huduma, kuzichakata na kutoa ripoti ambazo huwezesha TCRA kutekeleza majukumu yake ya udhibiti na kuhakiki taarifa za mapato kwa watoa huduma wa mawasiliano, hivyo kuwezesha serikali kukusanya mapato yake kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumza kuhusu kupungua kwa simu za kimataifa, Dk Bakari alielezea kuwa kupungua kwa simu hizo kumesababishwa na ongezeko la matumizi ya majukwaa ya mawasiliano ya kijamii.

“Dakika za simu za kimataifa zilizopokelewa zilipungua kwa asilimia 7.54 kutoka dakika 3,136,692 mwezi Julai 2022 hadi dakika 2,900,165 mwezi Juni 2023, wakati dakika za simu za kimataifa zilizotumwa zilipungua kwa asilimia 7.46 kutoka dakika 2,405,522 hadi dakika 2,226,071 kwa kipindi hicho hicho.

Kupungua kwa simu za kimataifa kunatokana na maendeleo ya teknolojia na upatikanaji wa chaguo mbadala za kupiga simu kupitia majukwaa ya intaneti kama vile WhatsApp, Facebook, Telegram, Zoom, na nyinginezo,”alisema Dk Bakari.

Alisema mbinu za kuzuia na hatua madhubuti za TCRA katika kudhibiti masuala ya vifaa vya mawasiliano havijaboresha tu usalama wa watumiaji na ubora wa vifaa bali pia vimesaidia kupunguza vitendo vya jinai vinavyohusiana na vifaa vya mawasiliano nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Uhalifu wa Mtandao wa Jeshi la Polisi, SSP Joshua Mwangasa, alipongeza TCRA kwa mchango wao mkubwa katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao.

Alisifu taasisi hiyo kwa kutoa teknolojia ya kisasa ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kazi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu wa mtandao kwa ufanisi.

“Kutokana na juhudi za TCRA, jeshi la polisi limeimarisha uwezo wake na kuhakikisha mazingira salama ya kidigitali kwa wananchi,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!