Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Biteko: Viongozi wa dini msichoke kuwaunganisha watu
Habari Mchanganyiko

Dk. Biteko: Viongozi wa dini msichoke kuwaunganisha watu

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Dk. Doto Biteko amewataka viongozi wa dini kutochoka kuunganisha watu ili kujenga Taifa lenye umoja, amani na mshikamano. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Biteko ameyasema hayo leo Jumatano kwenye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste ambao ulikuwa na lengo la kuombea Amani na Umoja miongoni mwa makanisa hayo.


Amesema Serikali inathamini mchango mkubwa unatolewa na viongozi wa dini nchini na kutoa wito kwa maaskofu wa Makanisa ya kipentekoste kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha amani inadumishwa.

“Nawapongeza sana Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste kwa Kuwa na Umoja na waumini wengi nchini wanaofikia takrbani milioni 12, pamoja na Umoja wenye nguvu na mshikamano,” alisema Dk. Biteko.

Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania-CPCT Askofu Dk. Barnabas Mtokambali, amesema Kuwa, viongozi wa dini wanathamini jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Kuhakikisha  demokrasa, utawala Bora na amani inadumishwa hapa nchini.

“Tunaipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanya kuhakikisha nchi iko kwenye utulivu, ustawi na amani na kuahidi kutoa ushirikiano pamoja na kuiombea Serikali.

Mkutano wa Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania ulianzishwa miaka thelathini iliyopita na ina jumla ya waumini milioni 12, na tayari madhehebu 28 yako mbioni kujiunga na Umoja huo  wenye jumla ya Wanachama 128.

Mkutano huo wa Umoja wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste CPCT umehudhuriwa na Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja huo Askofu Dk. Sylvester Gamanywa, Makamu Mwenyekiti wa CPCT Askofu Dk. Daniel Awet,  pamoja na Maaskofu kutoka Madhehebu mbalimbali chini ya umoja huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!