Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Rungwe apongeza mchango wa Wananchi katika ujenzi wa Shule ya Msingi na Bweni la Sekondari
Habari Mchanganyiko

DC Rungwe apongeza mchango wa Wananchi katika ujenzi wa Shule ya Msingi na Bweni la Sekondari

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amefanya ziara katika Kata ya Ikuti na kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wakazi wa kata hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Akikagua ujenzi wa shule mpya ya msingi katika Kijiji cha Ikuti pamoja hosteli ya wavulana katika Shule ya Sekondari Ikuti kwa nyakati tofauti, Haniu amepongeza wakazi wa kata hiyo kwa jitihada wanazozionesha katika kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo na kuwa hatua hiyo itaharakisha upatikanaji wa maisha bora kuanzia ngazi ya kaya na kata kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Haniu ameuagiza uongozi wa kata hiyo kuhakikisha unasimamia ipasavyo usomaji wa mapato na matumizi katika vijiji vyote ikiwa ni nyenzo muhimu katika utawala bora na Ushirikishwaji wa wananchi katika kufikia maamuzi ya maendeleo yao.

Pia, ametoa maelekezo kwa wakazi wa kata hiyo na wilaya kwa ujumla kushiriki katika mikutano ya hadhara ,kutoa maoni na kujadiliana bila kuathiri amani na utulivu na Kuwa viongozi wa dini na mila wana nafasi kubwa kutatua changamoto zinazowakabili badala ya kuanzisha na kushiriki katika migogoro mbalimbali.

Wakati huohuo ameagiza wazazi wote katika shule zote zilizopo katika Wilaya ya Rungwe kuhakikisha wanachangia chakula shuleni ili kuongeza ufaulu sambamba na kuondoa utapiamlo na udumavu kwa wanafunzi.

Hata hivyo, Haniu ameeleza kuwa haya yatawezekana iwapo wakazi wa wilaya ya Rungwe wataendelea kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa mvua na maji unakuwa endelevu mwaka mzima.

Katika ziara hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Renatus Mchau ambapo ametaja baadhi ya miradi inayotekelezwa katika kata hiyo kuwa ni pamoja Ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Sekondari Kyobo, Ukamilishaji wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Kyobo, Ujenzi wa vyumba viwili na vyoo katika Shule ya Msingi Ikuti na Kinyika pamoja na miradi mingine ya maji, umeme na barabara inayoondelea.

Ujenzi wa jengo la mionzi (X-Ray)
Aidha, ameagiza uongozi wa kata hiyo kukamilisha ujenzi wa jengo la mionzi (X-Ray) katika kituo hicho cha Afya Ikuti ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa ukaribu zaidi.

DC Haniu amesema: “Serikali yenu sikivu sana, imeshanunua kifaa hiki muhimu kwa matibabu ya wananchi, hivyo siyo vema tukashindwa kukitumia kwa kukosa jengo. Tafadhali tushikamane kukamilisha ujenzi huu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!