Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya DC Korogwe aibua mazito sakata la daktari aliyefumua mshono wa mgonjwa
Afya

DC Korogwe aibua mazito sakata la daktari aliyefumua mshono wa mgonjwa

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi
Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi amesema anachelea kuamini taarifa iliyotolewa na wizara ya afya kuhusu tukio la daktari aliyemfumua mshono mgonjwa kuwa ni taarifa rasmi kwa sababu wizara hiyo ndiyo ilipaswa kutoa majibu na sio kuuliza swali kwa Watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu. Korogwe … (endelea).

Mbali na kusitikishwa na tukio hilo, amesema serikali inayo mifumo yake kupata taarifa sahihi kupitia kwenye mifumo yake ya kiutendaji.

Mwanukuzi ametoa kauli hiyo baada ya jana tarehe 4 Septemba Wizara ya afya kueleza masikitiko yake kuhusu mtaalam mmoja wa afya(Jackson Silvanus Meli) aliyemshona mgonjwa jeraha na kisha kulifumua kwa madai kuwa hakuweza kulipa gharama.

Video ya mtaalam huyo kutoka kituo cha afya Kerenge kilichopo tarafa ya Magoma halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ilisambaa mitandaoni na kuibua hali ya sintofahamu.

“Ikiwa hili limetokea nchini basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu. Hivyo, wizara inaomba wenye taarifa za wapi au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya wizara ya afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya waziri wa afya ya 0734124191, ” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosambaa mitandaoni jana.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 5 Septemba, 2021 jijini Tanga, Mwanukuzi amesema “Wizara ya afya ndio inayotakiwa kutoa majibu kwa watanzania na sio kuuliza kwa watanzania kuhusu hatua hii.

“Kwa hiyo kama taratibu stahiki zingechukuliwa kutafuta hii taarifa, taarifa hii ingeweza kupatikana na nachelea kuamini ni wizara iliyotoa taarifa mitandaoni kwa sababu ndio iliyotakiwa kuchukua fursa hii kuwaeleza wananchi.

“Kutofanya hivyo ni kuichonganisha serikali ya Rais Samia na wananchi wake kuonekana kwamba serikali haifanyi kazi wakati iko mstari wa mbele kufanya kazi, kusimami haki na sisi kama wasaidizi wake tuko macho kufanya hayo,” amesema.

Hata hivyo, Mwanukuzi ameungana na Naibu katibu mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia afya, Dk. Grace Magembe kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 28 Julai, 2021.

Mbali na kukiri kutokea kwa tukio hilo, Mwanukuzi amesema tabibu Meli ambaye ni tabibu wa daraja la pili, tayari amechukuliwa hatua za awali.

“Hili tukio ni la muda mrefu lakini tunashangaa kwamba limetolewa kama ni jambo jipya. Baada ya taarifa hiyo kutokea moja kwa moja hatua zilichukuliwa.

“Serikali ya Rais Samia inatenda kazi kwa wajibu na ufanisi na sisi kama wasaidizi wake au viongozi tuko makini tukiona suala zito kama hilo halifai ndani ya jamii moja kwa moja bila kupoteza wakati tunachukua hatua stahiki,” amesema.

Amesema hatua zilizochukuliwa ni pamoja na tabibu huyo kukamatwa siku hiyohiyo ya tarehe 28 Julai na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

“Sambamba na kuwekwa chini ya ulinzi, halmashauri ilichukua hatua kumsimamisha kazi, taarifa zake zimeshawasilisha baraza la matibahu Tanzania kwa ajili ya kuchukua hatua zinazofuata kwa mujibu wa sheria kwani baraza ni mamlaka yake ya kinidhamu,” amesema.

Aidha, amewaomba wananchi kuwa watulivu na waelewe kwamba hatua zote zimeshachukuliwa kama ilivyopaswa na waendelee na shughuli zao kama kawaida.

“Nashukuru Tamisemi imechukua hatua stahiki kufuatilia na kutoa taarifa mtandaoni, nawapongeza Tamisemi kwani hicho ndicho kilichotokea.

“Taarifa ni ya siku nyingi lakini inatrend sasa hivi, kwa hiyo katika serikali ya Rais Samia haiwezekani matukio haya yakajitokeza bila sisi wasaidizi wake kuchukua hatua,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!