September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aeleza madhumuni kugeukia ‘Tour guide’

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema madhumuni makubwa ya mzunguko anaoufanya kwenye vituo vya utalii na rasilimali nyingine za Tanzania, ni kuionesha dunia vivutio na rasilimali zilizopo nchini.
Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Pia amesema kupitia filamu inayoandaliwa, Tanzania inakwenda kuuambia ulimwengu kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana hapa nchini.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Septemba 2021 alipotembelea eneo la machimbo ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara na kuzungumza na wananchi eneo hilo.

“Nina kazi maalumu humu ndani, mimi ni muongoza watalii yaani wale wazungu, mimi ninawaonesha hapa tunafanya hivi,” amesema.

Amesema madini hayo ya Tanzanite yana mwisho hivyo Watanzania wanatakiwa kuuza kwa mpangilio maalumu.

“Tukiuza ovyo tutayashusha thamani, tukiuza kwa mpangilio Tanzanite yetu itapata thamani.

“Tunakwenda kwenye maeneo mbalimbali ya vivutio ili kuionesha duniani kwamba Tanzania tuna rasilimali adimu za kuchangia uchumia duniani… tuna siasa safi na mazingira safi, hivyo wawekezaji waje.

“Hayo ndio madhumuni makubwa ya mzunguko wangu… tena nakwenda kuwaonesha na kuwalezea watalii mbalimbali ninaokutana kuhusu vivutio vyetu na rasilimali tulizonazo ndio maana nimevaa hata nguo za magwanda ya kitalii,” amesema Rais Samia.

Aidha, aliwaomba wananchi hao wa Simanjiro wavute subira kwani atapanga ratiba ya kufanya ziara rasmi ili kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Pamoja na mambo mengine amesema kuna changamoto katika Ukuta wa eneo la machimbo Mirerani pamoja na kitalu C.

Ameongeza kuwa tayari Mamlaka ya maeneo maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) imetoa eneo la hekari 250 kwa ajili ya ujenzi wa soko la madini hayo ya Tanzania.

“Soko tunakwenda kujenga katika eneo hilo, Tanzanite itachimbwa na kuuzwa hapa, niwaambie kwamba serikali tunajipanga tunajua matatizo na changamoto naomba tushirikiane, nipeni ushirikiano nami serikali yangu tuweze kutekeleza yale ambayo tumewaahidi,

“Najua changamoto haziishi kwa sababu watu tunazaliwa kila leo, lakini changamoto hizi tutazipunguza.

error: Content is protected !!