Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari DC Gondwe awafunda wanawake wajasiriamali
Habari

DC Gondwe awafunda wanawake wajasiriamali

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni (DC), jijini Dar es Salaam, Godwin Gondwe amewataka wanawake wajasiriamali, kusimamia malengo yao, kuboresha bidhaa wanazozalisha na kutumia vyema mitandao ya kijamii kupanua wigo wa soko. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza jana Jumapili, tarehe 5 Desemba 2021, katika hafla maalum ya kuwawezesha wanawake wajasirimali iliyoandaliwa na Taasisi ya Amka Twende, Gondwe alisema mara baada ya kutembelea bidhaa katika shughuli hiyo, “nimeona mna bidhaa za viwango sana.”

Alisema, bidhaa hizo mbalimbali, zinapaswa kuwa “branding, kwani hili linakosekana kwenye bidhaa nyingi sana. Lakini, uwe na logo na vifungashio vizuri, ili kuendelea kuwavutia watu wa ndani na nje ya nchi.”

“Tuongeze wigo wetu wa bidhaa tunazozalisha kwa kupanua masoko mengi zaidi ili kuongeza kipato na fedha kwa wananchi na ninyi wenyewe. Kipato cha mama, huwa hakitoki hovyo hovyo bila mpangilio, tunawaamini, simamieni hili,” alisema

Kuhusu mitandao ya kijamii, Gondwe alisema “tuongeze wigo wa masoko, tutumie mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zetu, lakini tutengeneze hata application yenu. Mkatengeneza shooping zenu mbalimbali, watu wa ndani na nje wakanunua.”

Huku akishangiliwa na wanawake hao, Gondwe alisema “mnapaswa kuwa na lugha nzuri kwenye biashara na yote kwa yote simamieni malengo na ndoto zenu. Wapo watakaowarudisha nyuma, msikubali, songeni mbele zaidi.”

Aidha, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanawake hao kujiunga katika vikundi ambavyo vitasajiliwa katika halmashauri ili wapatiwe mikopo kupitia asilimua kumi za mapato ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

“Sisi Kinondoni, mapato yetu kwa mwaka ni Sh.49 bilioni, kwa hiyo jiungeni na ninawapa siku 14 mkamilishe hili ili tukitoa hii mikopo, iwafikie na ninyi. Rais Samia Suluhu Hassan ndiye lengo lake, kuwawezesha, sasa changamkieni fursa,” alisema Gondwe

Naye Mwenyekiti wa Amka Twende, Upendo Mwalongo alisema, wamepokea maelekezo ya mkuu huyo wilaya na wanakwenda kujipanga ili kuchangamkia fursa hiyo.

Upendo alisema, Amka Twende ni kikundi cha akina mama wajasiriamali ambao wamejenga mtandao mkubwa kwenye sekta ya biashara na maendeleo ya jamii.

Alisema Desemba 2019, walifanya harambee na kupatikana Sh.15 milioni na kuwapatia wajane wa Wilaya ya Temeke, waliokuwa wakiishi na virusi vya Ukimwi ambao pia, walikuwa wakiishi katika mazingira magumu.

Alisema Desemba mwaka jana, walifanya bonanza kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa shule ya Sinza Maalum, wilaya ya Kinondoni ili kukidhi mahitaji yao ikiwemo ujenzi wa vyoo na ukuta wa shule.

Upendo alisema, bonanza hilo lilikusanya Sh.11 mlioni “zilizpatyikana na kukabidhi kwa shule ya watoti wenye ulemavu wa Sinza.”

“Mwaka huu, tumemkabidhi Sh.3 milioni, mkuu wa wilaya ili kuunga juhudi za Rais wetu, Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa miundombinu ya shule. Tumezoea akija mgeni rasmi tunalia shida, sasa hapana, tunatoa na sisi,” alisema Upendo

Kwa upande wake, Buturi Suna kutoka Benki ya NMB alisema “sisi kila sehemu kama benki tupo ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za kibenki. Kuna mikopo ya wajasiriamali, hivyo ichangamkieni.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!