Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DC aongoza kupanda miti 1,000 Rungwe kwa siku moja, mbolea, ruzuku kuendelea kusambazwa
Habari za Siasa

DC aongoza kupanda miti 1,000 Rungwe kwa siku moja, mbolea, ruzuku kuendelea kusambazwa

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu ameongoza zoezi la Upandaji miti katika Kijiji cha Ijoka, Kata ya Mpombo Halmashauri ya Busokelo ikiwa ni hatua muhimu ya kulinda vyanzo vya maji, kudumisha uoto wa asili, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Jumla ya miti 1000 imepandwa leo Februari 6, 2023 katika eneo hilo huku malengo yakiwa ni kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho, Haniu ameagiza wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wa wanapanda miti mara kwa mara sambamba na kuepukana na tabia ya ukataji miti hovyo, kuchoma moto, kulima kando ya vyanzo vya maji na kuchunga Mifugo kwenye hifadhi za maji.

Aidha, amewahakikishia wakazi wote wa Wilaya ya Rungwe kuwa Mbolea ya Ruzuku imeendelea kusambazwa katika maeneo yote kwani Serikali kupitia Wizara ya kilimo imeboresha mazingira ya Kilimo na hivyo kila mkazi atapata pembejeo hiyo muhimu kwa maendeleo endelevu nchini.

haniu-zungu-jpg.2508546.jpg

“Niagize kila kata kuwe na ratiba maalumu inayoonesha ni lini mbolea inaletwa katika kata husika ili kuwaondolea adha wananchi kufuata huduma umbali mrefu huku wakipoteza muda mwingi wa uzalishaji,” ameagiza Haniu.

Pamoja na hiyo ameagiza mawakala wote wa usambazaji wa Mbolea kuacha kuuza mbolea kwa magendo kwani kufanya hivyo kunaondoa nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Watanzania wanazalisha kwa tija na maendeleo bila vikwazo vyovyote.

Katika hatua nyingine Haniu ametoa maelekezo kwa wazazi wote kuhakikisha watoto wao waliofikisha umri wa kwenda shule sambamba na kujiunga na kidato kwanza wanawapeleka mapema kwani kufanya hivyo itasaidia kupata huduma hiyo muhimu kwa Ustawi wa Mtoto.

Halmashauri ya Busokelo imeandikisha watoto wa darasa la kwanza na wali kwa zaidi ya asilimia 100% huku uandikishaji ukiendelea

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!