Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Miaka 46 ya CCM hakuna Mtanzania atayekufa njaa – Bashe
Habari za Siasa

Miaka 46 ya CCM hakuna Mtanzania atayekufa njaa – Bashe

Mahindi yakiwa shambani
Spread the love

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amesema hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa na Serikali haitafunga mipaka ya nchi kwa kuzuia mfumuko wa bei ya chakula uliopo kwa sasa bali itapunguza gharama za pembejeo na kumpa mkulima nafasi ya kupata faida ya Kilimo. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Waziri Bashe alisema hayo jana mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo alipokuwa akimalizia ziara yake ya siku 9 mkoani Morogoro kwenye  maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika mkoani hapa.

Bashe alisema Mfumuko wa bei Kwenye Sekta ya kilimo ulitengezwa kikoloni tangu nchi ilipopata Uhuru sababu Ilikuwa mazao ya wakulima yakivunwa yanakuwa mazao ya Taifana kupangiwa bei na pa Kuuza lakini kwa Sasa mazao ya wakulima ni ya wakulima kama lilivyo duka la Mangi.

“Muda wa kufanya mkulima kama mtumwa alime yeye na familia yake akivuna tu mnaingilia na kumwambia hatakiwi kuuza wakati Ile ni mali yake kama rahisi nendeni nanyi mkalime” Alisema.

Alisema Serikali imechukua njia mbili katika kuondoa suala la mfumuko wa bei wakianza na kununua mazao ya wakulima na baadae kuyaingiza sokoni pale panapokuwa na njaa ambapo hivi karibuni wataingiza tani 46,000 za mahindi ambayo hawayauzi kwa wafanyabiashara bali wananchi.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Naye Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdulaziz Abood katika kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) ametumia jumla ya shilingi mil 50 kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwenye Sekta ya elimu ya sekondari na msingi ikiwemo kuwalipia ada wanafunzi ya 300 wa vyuo vikuu.

Alisema anamshkuru Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuwapatia kiasi cha sh. bil 10 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya elimu na Afya Wilayani humo.

Alisema katika kutekeleza Ilani katika Sekta ya elimu ya sekondari namsingi ametumia zaidi ya mil 50 ikiwemo kuwalipia ada wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vikuu.

Alisema fedha hizo zimekwenda katika miradi ha Elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara 6 shule sa sekondari, bweni la shule ya msingi kihonda na vyumba 20 vya madarasa.

Aidha alisema jumla ya Vikundi 576 vya ujasiriamali vimesaidiwa kimikopo na kukuza uchumi wao Manispaa na kuendelea.

Hata hivyo alimshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuahidi kutatua kero ya maji Mkoani hapa na kuhakikisha tatizo hilo linaisha kabisa hadi kufikia mwaka 2020/25 kuwa yanapatikana.

Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa alisema Serikali inatarajia kujenga hospitali kubwa na ya kisasa ya Rufaa kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali na hospitali iliyopo kubaki kuwa hospitali ya Wilaya.

Akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro Katibu Mkuu CCM Taifa Daniel Chongolo alisema katika kuadhimisha miaka 46 ya CCM ni kumbukumbu ya kuangalia ahadi zilizotolewa na Chama kupitia ilani ake ya mwaka 2020/25 zinazoendelea kutekelezwa ili kutatua changamoto mbalimbali ndani ya mkoa wa Morogoro na Tanzania nzima kwa ujumla.

Alisema jumla ya sh bil 500 zimetolewa na Serikali ndani kwa mkoa wa Morogoro ili kutatua changamoto ikiwemo miundombinu ya maji na umeme na katika sekta mbalimbali.

Aidha aliwaasa wakazi wa Morogoro licha ya kuwa na mito mingi ambayo ndio vyanzo vya maji wanapaswa kuitunza ili vyanzo hivyo viendelee kuwa na maji.

Hata hivyo aliwataka viongozi kusimamia na kutoa mifugo vamizi kwenye maeneo ya wakulima ili kuwe na amani inayohitajika.

Akizungumzia masuala ya maji Naibu Waziri wa maji Mary – Priscar Mahundi  alisema wizara inajipanga kusambaza maji majumbani kote ikiwa na umbali si chini ya mita 400 ili kuokoa ndoa za kinamama na kusogeza huduma kwa jamii.

Alisema kinamama wengi wamekuwa wakipoteza ndoa zao kwa kutembea umbali mrefu kutafuta maji na hivyo Rais ameliona hilo na kulipatia ufumbuzi.

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Naye Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI David Silinde alisema jumla ya sh bil 117 zimeshafika kwenye halmashauri kuhakikisha Tarafa zote zinakuwa na vituo vya afya na Halmashauri 28 kupatiwa hospitali za ngazi ya Wilaya nchini.

Akizungumzia uhaba wa vifaa vipimo na tiba kwenye vituo vya afya Mahundi alisema, Rais  Dk. Samia Suluhu Hassan alitoa kiasi cha sh. bil 15.7 kwa ajili ya vifaa saidizi na tiba ambavyo vyote tayari vimeanza kuingia na vitagawiwa kama inayopaswa.

Hivyo alisema TAMISEMI itahakikisha fedha zote zinazoshuka chini kwa ajili miradi zinafanya kazi ilivyokusudiwa bila kuwepo kwa mianya yoyote ya kupotea.

Naye katibu wa siasa itikadi na uenezi Taifa Sophia Mjema aliupongeza mkoa na Chama kwa kuweza kusimamia ilani ya CCM na kufanya kuwa na wanachama wengi wenye mshikamano katika mambo mengi ikiwemo sherehe za kuzaliwa CCM miaka 46.

Alisema Ilani ya CCM inaendelea kutekelezwa hasa katika kujenga miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu, Afya na maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!