Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria
Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love

 

WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi lenye kipimo cha 7.8, lililotokea leo tarehe 6 Februari 2023, katika mpaka wa nchi ya Uturuki na Syria. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa tukio hilo, imeelezwa kuwa zaidi ya watu 50 katika idadi hiyo wamefariki dunia upande wa Syria.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Suleymon Soylu, amesema miji 10 nchini humo imeathirika na tetemeko hilo, ikiwemo Gaziantep, Kahramanmaras, Hatay, Osmaniye, Adiyaman, Malatya, Sanliurfa.

Pia imeripotiwa kuwa majengo mengi yameporomoka na kwamba timu za uokoaji zimetumwa kutoa msaada kwa manusura wa tetemeko hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!