Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko CWHRDs kuweka mikakati kuimarisha harakati za wanawake wanaotetea haki
Habari Mchanganyiko

CWHRDs kuweka mikakati kuimarisha harakati za wanawake wanaotetea haki

Spread the love

Mtandao wa wanawake watetezi wa haki za binadamu Tanzania (CWHRDs TZ), umeendesha mkutano wake mkuu uliolenga kuweka mikakati ya kuimarisha harakati za kundi hilo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es salaam…(endelea) .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CWHRDs TZ, mkutano huo wa nne (2023-2024) umefanyika leo Jumamosi, tarehe 6 Aprili 2024, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umewakutanisha wanachama zaidi ya 70 kutoka Tanzania Bara, Unguja na Pemba visiwani Zanzibar, ambao wamepata fursa ya kujadili maendeleo ya mtandao kwa 2023 na kupanga mikakati ya mtandao kwa 2024.

“Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa na wanawake watetezi wa haki za binadamu katika mkutano huo, ni pamoja na hatua zitakazotekelezwa na sekretarieti ya mtandao katika kukuza na kuuimarisha harakati za kuwawezesha wanachama kukua katika maeneo mbali mbali ikiwemo  usimamizi mzuri wa fedha, pamoja na kuunda timu zenye weledi zitakazoewezesha mashirika wanachana kujiimarisha kikanda,” imesema taarifa hiyo.

Sambamba na mkakati huo, washiriki wamejadili mbinu zitakazotumika na mtandao katika kuimarisha harakati za wanawake watetezi,kuwajengea uwezo na  kukuza ulinzi na usalama wa mazingira ya kazi kwa wanawake hao, pamoja na kuwafahamisha mbinu za kujilinda pindi wanapotekeleza majukumu yao katika maeneo hatarishi.

Mtandao wa CWHRDs TZ, ulianzishwa 2019 kwa malengo ya kuwajengea mazingira salama na kuimarisha jitihada na harakati za wanawake watetezi wa haki za binadamu Tanzania, katika kuhakikisha mwanamke na mtoto anakuwa huru dhidi ya ukandamizaji wowote  wa haki za binadamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!