Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Chama, Miquisone waingia kikosi bora cha wiki Afrika
Michezo

Chama, Miquisone waingia kikosi bora cha wiki Afrika

Clatous Chama
Spread the love

 

WACHEZAJI wawili wa kikosi cha Simba, Clatous Chama na Luis Miquisone wameingia kwenye kikosi cha kwanza cha wiki barani Afrika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikosi hiko ambacho kina wachezaji 11, ambao wamefanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika michezo ya makundi iliyopigwa hivi karibuni.

Wachezaji hao wameingia kwenye kikosi hiko baada ya kuonesha kiwango kizuri kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambapo Simba iliminyana dhidi ya AS Vita kutoka Jamhuri ya Congo.

Kwenye mchezo huo wa kundi A, uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Simba walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 4-1 na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Luis Miquisone

Katika ushindi huo wa mabao 4-1, wachezaji hao wawili walihusika moja kwa moja kwenye mabao hayo manne.

Chama alifanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi ya goli moja (assist), huku Miquisone akiingia kambani mara moja.

Wakati huo huo, Chama amewekwa kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki pamoja na wachezaji Ricardo Goss wa Mamelodi Sundown, Amir Sayoud wa CR Belouizdad na Ferjani Sassi.

Katika kinyang’anyiro hiko Chama anaongoka akiwa na asilimia 51 baada ya kupigiwa kura nyingi kuliko wengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!