Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Rais Samia aanzisha salamu mpya
Habari

Rais Samia aanzisha salamu mpya

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameanzisha salamu mpya ambayo atakuwa akiitumia katika shughuli mbalimbali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Samia ametambulisha salamu hiyo leo Jumanne, tarehe 6 Aprili 2021, Ikulu ya Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza kuwaapisha makatibu wakuu saba, naibu wao tisa na wakuu wengine wa taasisi.

Mara baada ya kumaliza kuwaapisha, amesema “nina salamu mpya, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtaitikia kazi iendelee.”

Katika hotuba yake, amekuwa akizungumza na kusema “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” waliohudhulia hafula hiyo wanaitikia “kazi iendelee.”

Makatibu wakuu walioapishwa ni, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Mpawe Tutuba; Mhandisi Leornard Robert Masanja (Nishati); Dk. Allan Herbert Kijazi (Maliasili na Utalii); Prof. Godius Kahyarara (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji) na Dk. Abel Makubi (Wizara ya Afya).

Wengine ni, Gabriel Joseph Migire (Uchukuzi) na Mary Maganga (Ofisi Makamu wa Rais).

Manaibu Katibu wakuu ni, Grace Maghembe Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya); Khatib Kazungu (Fedha na Mipango). Mohammed Abdallah Khamis (Ofisi Makamu wa Rais-Muungano).

Na Prof. Jamal Adam Katundu na Caspary Caspary Muya Manaibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Wengine ni, Balozi Fatma Rajab (Mambo ya Nje). Dk. Hashil Twaibu Abdallah (Viwanda na Biashara). Dk. Carolyne Ignatius Nombo (Elimu ya Msingi, Sekondari na Ufundi Stadi). Kheri Abdul Mahimbali (Nishati)

Paulina Mkwama, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Waalimu.

Wakuu wa taasisi walioapishwa ni, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifello Wedson Sichwale. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alhayo Japan Kidata na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya , Gerald Kusaya Musabila.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabir Bakari Kuwe. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) , Masha John Mshomba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Erick Benedict Hamis.

Wengine ni, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!